Polisi Simiyu wakamata majangili 9 waliotungua helkopta na bunduki 27, Risasi 105.


Siku chache baada ya watu wanaosadikiwa kuwa majangili kuitungua helkopta ya kampuni ya uwekezezaji ya Mwiba Holidings iliyoko wilayani Meatu mkoani Simiyu na kuuwa rubani mmoja, Rogers Gower raia wa Uingereza, jeshi la polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kuwakamata majangili 9 akiwemo jangili mmoja aliyekiri kufanya tukio hilo pamoja na vipande vitatu vya meno ya Tembo.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu kamishina msaidizi wa polisi Lazaro Mambosasa anaelezea kukamatwa kawa majangili hao.
Aidha kamanda Mambosasa amesema sambamba na kukamatwa kwa majangili hao pia wamefanikiwa kukamata bunduki 27 na risasi 105 ambazo zilikuwa zinamilikiwa kisheria lakini zilikuwa zinatumika kinyume cha sheria ambapo miongoni mwa bunduki hizo ni ile iliyotumika katika kutungua helkopta hiyo.
Kwa upande wake Mhifadhi mkuu wa Serengeti William Mwakilema amelipongeza jeshi la polisi ambapo amesema tukio hilo lilipotokea liliwasikitisha sana kwani hasara ilipatikana kutokana na kutunguliwa kwa helkopta.

Theme images by hanoded. Powered by Blogger.