NJOMBE WAZUIA UIGIZAJI WA MAZAO KUTOKA MIKOA MINGINE SABABU NI HII
msimamo wa serikali mkoa wa Njombe ni marufuku uingizwaji wa mazao ya chakula mkoani humo shughuli ambyo wakazi wa mkoa huo wanauwezo wa kufanya.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr, Rehema Nchimbi
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi amesema mkoa wake
hautaruhusu uingizwaji wa mazao ya chakula kutoka nje ya mkoa huo kwani mkoa huo unaweza kuzalisha wenyewe chakula cha kutosha na hata kuuza.
Kauli ya dr Nchimbi inakuja kufuatia uwepo wa mkoa huo kuwa na utajiri wa madini ya liganga na mchuchuma mgodi ambao unatarajiwa kuingiza zaidi ya wageni 3000 kufanya shughuli za uchimbaji.
Kutokana na faida hiyo ya uingiaji wageni hao ni fursa sasa ya wakazi wa Njombe kuuza chakula chao na kufanya biashara pia huku wakitakiwa kuchangamkia fursa hiyo na kutokuendelea kushuhudia mazo yakiingizwa kutoka mikoa mingine.
Kauli ya Nchimbi imetolewa katika kilele cha maazimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ccm akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo wilayani Njombe.
Shutuma za baadhji ya wakazi na wananchi wa Njombe kwamba wao wanauwezo wa kuzalisha chakula mabcho kinaweza kulisha Tanzania Nzima lakini wanakabiliwa na changamoto za bei huku wakitaja mfano wa soko la viazi ambalo wanunuzi hawakubali kununua bila rumbesa.
Mtazamo wao wanaonelea ni vema serikali ishikiliea msimamo huo wa kutokuruhusu mazao ya nje na kuendelea kuomba kujengwa kwa viwanda vya usindikaji mazao hayo hasa Unga.