Niliaibika Sana, Sitakaa Nisahau

Nakumbuka nilipokuwa primary kipindi hiko nilikuwa na girlfriend wangu ambaye tulikuwa tunaishi jirani na tunasoma shule moja, darasa moja na dawati moja. Kila siku tulikuwa tunaenda shuleni pamoja na tunarudi pamoja nyumbani.

Ulikuwa ukinikosa nyumbani basi ujue nko kwao, na kila weekend tulikuwa tunashinda pamoja mpaka tunasahau kama kuna kula. Nakumbuka baba angu alikuwa akinigombeza kuwa nmezidisha michezo sana mpaka perfomance yangu class ikawa inashuka na kusahau hata muda wa kurudi kula kisa michezo.

Sasa siku moja jumapili niliangalia movie sana mpaka mida ya saa 9 za usiku ndo nkaenda kulala, sasa asubuhi yake niliamka mchovu na nikakumbuka ni siku ya shule ikanibdi niende japo nilikuwa nasinzia sana njani huku nikielekea school.

Baada ya kufanya usafi tukaingia class. NILIKUWA NIPO DARASA LA TATU KIPINDI HICHO.
Sasa tulipoingia tena class saa 13:00 baada ya kutoka lunch, tena lunch yenyewe ni makande na jinsi maharage yalivyokuwa na usingizi.

Nikawa NASINZIA mbayaa ukijumlisha tena na jana Kuchelewa kulala ndo ikawa balaa sana. ilikuwa ni somo la English hvyo teacher alivyoingia na kuanza kufundishwa nikawa nimepitiwa na usingizi baada ya ule uchovu mkali.

Punde kidogo nkashtushwa na yule girlfriend wangu kuwa teacher alikuwa amenipoint mm nijibu swali. aaaagrrh! hapo nkashtuka balaaa alafu na hata hili swali lenyewe nlikuwa sijui kaulizaje. basi nikawa nabababika tuu mara teacher akarudia tena kuuliza "what the meaning of TOGETHER?"

Basi nkawa nababaika bila kujua nijibu vipi ila nkasikia yule GF wangu akiniambia kwa mbali "jibu lake ni TUNAWAKILISHA"Heeeeh! basi na mimi ikavuta picha huku nikipambanua lile jibu nililolisikia nikalicombine na lile neno ka kwenye Chanel 5 kuwa wanaandikaga "TOGETHER, TUNAWAKILISHA" basi hapo nikaona Ewaaah! hili ndo jubu, nikajibu kwa sauti kubwa huku nikihiamini kuwa jibu lake ni TUNAWAKILISHA.

Heeh! mara nikasikia kila mtu kaduwaa baada ya hapo wanafunzi pamoja na mwalimu wakacheka mbayaaaa.Basi hyo siku nilichekwa sana karibia siku nzima mpaka nikawa sina raha. keaho yake pia nilipikuja shule wakawa tayari wameshanibatiza jina naitwa TUNAWAKILISHA. ikawa kila mahali nikipita naitwa tunawakilisha, tubawakilisha mpaka jina nikalizoea mpka namaliza darasa la 7 nikawa naitwa hivyo hvyo Tunawakilisha.Tunawakilisha.

YANI ILIKUWA NI AIBU AMBAYO MPAKA SASA HIVI NAONA IMEZIDI KULIKO AIBU ZOTE ZILIZOWAHI KUNIPATA.Je na wewe mdau unakumbuka ulipikuwa scul ni aibu gani ilishawahi kukupa/kukumba?

Theme images by hanoded. Powered by Blogger.