MSIMAMO WA LIGI YA VODACOM BAADA YA MECHI ZA LEO
Baada ya kupokea kichapo katika michezo yake miwili iliyopita, hii leo Mbeya city wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 mbele ya JKT Ruvu katika mchezo ulioanzaa saa tisa mchana katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom Mbeya city walikuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Hassan Mwasapile katika dakika ya 20 ya mchezo huo.
Mbeya city waliandika goli la pili katika kipindi cha pili kupitia kwa Yohana Morice na kupelekea mchezo kumalzika kwa Mbeya city kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Katika mchezo mwingine uliochezwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani Ndanda FC wamewafunga wenyeji wao Coastal union goli 1-0, goli lililo fungwa na mchezaji wa Azam FC aliye kwa mkopo Ndanda FC, Bryson Raphael.
MATOKEO YA MICHEZO YA LEO
JKT RUVU 1-2 MBEYA CITYCOASTAL UNION 0-1 NDANDA FC