MBEYA CITY WAWA WA MWISHO KUTINGA 16 BOTA KOMBE LA TFF

Timu ya Mbeya City imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya kombe la TFF linalodhaminiwa na Azam Sports, baada ya leo kuwafunga jirani zao Wenda FC kwa mikwaju ya penati.
Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Sopkoine ulishuhudia Mbeya city na Wenda FC kumaliza dakika 90 bila ya kufungana na mikwaju ya penati ikachukuwa hatima ambapo Mbeya City walifanikiwa kupata pennati 5 dhidi ya 4 za Wenda FC.
Matokeo hayo inaifanya Mbeya city kuwa timu ya 16 kufuzu hatua hiyo ambayo ratiba yake imetoka leo.