Mbaroni kwa Unyang’anyi, Kujeruhi


JESHI la Polisi mkoani Tanga linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuvamia jengo la biashara na kujeruhi watu watatu kwa risasi akiwamo askari wakati wakifanya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Watu hao walivamia nyumbani kwa mfanyabiashara Zuheri Taibal (43) mkazi wa Kata ya Ngamiani Kati jijini hapa katika Mtaa wa Barabara ya Sita kwa Barabara ya Jamaa ambako ndipo anapofanyia shughuli za biashara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Mihayo Misikhela alithibitisha tukio hilo na kusema ujambazi huo ulifanyika jana saa sita mchana wakati majambazi watatu walipomvamia mfanyabiashara huyo kwa kutumia silaha.

“Kwenye uvamizi huo majambazi hao walifanikiwa kupora fedha taslimu kiasi cha shilingi laki mbili na kujeruhi watu watatu akiwemo askari wetu wa Jeshi la Polisi,” alisema Kamanda Misikhela.

Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni askari Koplo George wa Kituo cha Polisi cha Chumbageni na raia wawili, Saleh Kassim (42) mkazi wa Kata ya Tangasisi aliyeumia sehemu za tumboni upande wa kushoto na Abdi Mussa `Seif’ (19), dereva wa bodaboda ambaye pia amejeruhiwa tumboni.



Kamanda alisema jambazi aliyejeruhiwa na baadaye kufa amefahamika kwa jina la Mathias Mntangi (32) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Magomeni jijini Tanga.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.