MATOKEO YA LIGI YA VODACOM MECHI ZA LEO




Mabinwa wa ligi kuu ya vodacom Yanga SC wameacha pointi 2 katika uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya baada ya leo kuabulia sare ya goli 2-2 toka kwa Tanzania Prisons katika mchezo wa 17 wa ligi kuu ya vodacom.

Katika mchezo huo ambao ulitawaliwa na mipira mirefu na kupeleka magoli matatu katika mchezo huo kufungwa kwa mipira ya kichwa kutokana na baadhi ya maeneo kuwemo na matope.

Yanga SC ndio waliofika kwa wingi langoni mwa Tanzania Prisons katika vipindi vyote viwili na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga magoli na kama wangekuwa makini basi wangetoka na ushindi wa goli 4 katika mchez huo wa leo.

Yanga SC ndio walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 36 kupitia kwa Amisi Tambwe akimalizia vyema krosi ya Haruna Niyonzima na kuipa yanga goli la kuongoza.

Kabla ya kuingi kwa goli hilo dakika 5 Nyuma beki wa Tanzania Prisons ilibidi kufanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliokuwa unaeleka golini mwao baada ya kipa wa timu hiyo kupotea.

Kazi nzuri ya Mohammed Mkopi inamaliziwa vyema na Jeremia Juma na kuisawazishia Tanzania Prinson goli katika dakika ya 40 na kupeleka mchezo kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Katika kipindi cha yanga walikuja kwa kasi, wakati Tanzania prisons wakibaki nyuma na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza ambapo katika dakika ya 62 walifanikiwa kupata faulo ambayo iliungwa vyema kwa kichwa na Mohammed Mkopi na kuiandikia Tanzania Prisons goli la pili.

Kuingia kwa goli hilo kulipoteza utulivu kwa yanga na kuanza kushambulia lango la Prisons kwa kasi na kama Prisons wangekuwa makini katika mashambulizi yao mawili ya kushtukiza basi hali ingekuwa tofauti hii leo.

Katika dakika 86 mwamuzi anaipatia yanga SC penati ambayo katika dakika ya 87 Saimon Msuva anaisawaizshia yanga sc goli hilo kwa mkwaju wa penati na kupelekea mchezo kumalizka kwa sare ya goli 2-2.

Kwa matokeo hayo yanga sc wanaambulia sare ya pili toka kwa Tanzania prisons msimu huu na hivyo kuvuna pointi 2 tu na kupelekea wakae kileleni kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Azam FC.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.