LIST YA WANAUME WALITOKA NA WEMA NDANI YA MIAKA YAKE 10 YA USTAA
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Mwandishi Wetu, AMANI
DAR ES SALAAM: Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ (27), ametimiza miaka 10 ya ustaa wake tangu alipotwaa Taji la Miss Tanzania, mwaka 2006 hadi mwaka huu 2016 ambapo upande wa pili wa maisha yake ya kimapenzi ulibebwa na mtungo wa wanaume alioingia nao kwenye uhusiano, Amani lina ripoti kamili.
Wema aliyezaliwa Septemba 28, 1989 akiwa mtoto wa mwisho kati ya mabinti wanne kwenye familia ya marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu kwa mkewe, Miriam Sepetu, mbali na ulimwende, pia ametikisa kwenye sinema za Kibongo, matangazo na runingani huku akipendwa na sehemu kubwa ya jamii.
….Akiwa na Idris.Wema mwenye sauti ya kitoto miaka yote, aliibuka kidedea kwenye Miss Tanzania mwaka huo akiwagaragaza Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Lisa Jensen.
AANZIA KWA MR BLUE, TID
Maisha yake ya kimapenzi ya awali, Wema alidaiwa kuwa ‘klozi’ na mastaa wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue’ na Khaleed Mohamed ‘TID’ kabla ya kuingia kwenye uchumba rasmi na aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’.
…NA KANUMBA
Katika kipindi cha uhusiano wake na Kanumba, mambo yalikwenda sawia ambapo kila walipokatiza mjini nyota zao ziling’aa huku wakishirikiana kutengeneza sinema zilizopendwa na mashabiki wao kama Red Valentine, White Maria na nyinginezo.
Wema akiwa na Luis.Hata hivyo, baada ya kipindi kirefu cha mapenzi ‘shatashata’, Wema na Kanumba walimwagana baada ya mwanadada huyo kuvunja vioo vya gari ya jamaa huyo na kufikishana polisi.
…NA JUMBE YUSUF JUMBE
Baada ya kunyanyua nyayo kutoka kwa Kanumba, Wema anayetajwa kuwa na roho ya kujali watu wasiojiweza, aliangukia kwenye penzi la mjasiriamali, Jumbe Yusuf Jumbe ambaye walitangaza ndoa kabla ya mama wa mrembo huyo kuingilia kati na kumchukua mwanaye mikononi mwa jamaa kwa kutumia nguvu ya ziada ambapo ilibidi Wema atupwe rumande ili kuweka akili yake sawa.
…NA CHAZ BABA
Wema hakuishia hapo kwani baada ya kuchomolewa kimabavu kwa Jumbe, alizama kwenye ‘mahaba niue’ na staa wa muziki wa Dansi Bongo, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’.
….Akiwa na Mond.Ni katika kipindi hicho ambapo familia ya Wema iliona ili kumnusuru ni bora akaishi na kusoma kwa dada yake nchini Marekani hivyo kuvunja penzi lake na Chaz Baba.
…NA DIAMOND PLATNUMZ
Akiwa nchini humo, ndipo Wema alipoanza kuchati na staa mwingine wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupitia Mtandao wa Kijamii wa Facebook ndipo wakaanzisha penzi lililokuwa gumzo mitandaoni kabla ya kuonana.
Alipotua Bongo, Wema akatua rasmi mikononi mwa Diamond na kuanza maisha ya pamoja yaliyojaa kila aina ya bashasha za ‘kimalovee’ hadharani huku wakimwagana na kurudiana mara kadhaa kabla ya kuachana jumla.
…NA KIGOGO CK
Baada ya kuachana na Diamond, Wema ambaye amekuwa akisaidia sana jamii, aliripotiwa kutoka kimapenzi na wanaume wengine kadha wa kadha akiwamo yule kigogo wake maarufu kwa jina la CK, mastaa wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’ na Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
…NA NAGARI KOMBO, MNAMIBIA
Wengine ni kijana wa mjini hapa Bongo, Nagari Kombo almaarufu ‘Staa wa Kaka’, jamaa aliyepata umaarufu kupitia Shindano la Big Brother Africa (BBA) ‘Hotshots’ 2014, Luis Mnana ambaye ni raia wa Namibia kisha kudaiwa kutoka na mbunge wa chama tawala cha CCM.
Wakati mashabiki wake wakiwa na maswali lukuki baada ya kuenea kuwa ni mjamzito na yeye mwenyewe akifurahia kuondokana na masengenyo kuwa ni mgumba ndipo akaibuka mshindi wa BBA 2014, Idris Sultan na kutangaza ndiye mwenye ujauzito huo na mmiliki halali wa mwanadada huyo.
MKONGO NAYE
Huyu naye alidaiwa kuwa na uhusiano na Wema ambapo kwa muda mfupi tu, habari zao zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na magazetini. Wema alidaiwa kumpata Mkongo huyo akiwa mikononi mwa staa mwenzake wa sinema Bongo, Jacqueline Wolper.
AWEKA REKODI
Kwa mujibu wa wachambuzi wa skendo za mastaa ndani na nje ya Bongo, Wema ameweka rekodi ya kuwa na wanaume wengi hata kuliko mwanamitindo na mtangazaji wa runinga nchini Marekani, Kim Kardashian ambaye kabla ya kutulia na Kanye West, alikuwa moto wa kuotea mbali.
Wadau wake wameliambia Amani kuwa, Wema ndiye staa pekee Bongo kipenzi chao ambaye ameweza ‘kumeinteini’ jina lake bila kushuka ndani ya Bongo na sasa amevuka mipaka kimataifa ambapo ukitaja jina la Wema Sepetu anafahamika vilivyo.
WEMA ANAJISIKIAJE?
Amani lilimtafuta Wema ili kujua anazungumziaje safari yake ya ustaa wa miaka 10 huku akiwa na msururu mrefu wa wanaume ambapo simu yake iliita bila kupokelewa lakini watu wake wa karibu walipofikiwa na gazeti hili walidai Madam kwa sasa anatumia muda mwingi kulea ujauzito wa uzao wake wa kwanza alioutafuta kwa muda mrefu.
SASA AMETULIA NA IDRIS WAKE
Kwa mujibu wa watu wake hao wa karibu, kwa sasa Wema ametulia tuli kama maji ya mtungi kwa Idris akisubiri kulea staa mwingine atakayezaliwa