KUTANA NA DIWANI WA CHADEMA ANAYEMSIFIA MAGUFULI


DIWANI wa Kata ya Hembeti wilayani Mvomero kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Mdidi amesema licha ya kuwa mpinzani, anamkubali Rais John Magufuli kutokana na utendaji wake wa kazi unaolenga kuimarisha uwajibikaji wa viongozi na watendaji katika kuwahudumia wananchi.

Amesema anamkubali kwa asilimia 100 Rais Magufuli kutokana na falsafa yake ya ‘Hapa Kazi Tu’, inayoendana na uchukuaji wa hatua mbalimbali za kinidhamu kwa watendaji wa serikali wanaobainika kwenda kinyume cha maadili na kutowajibika ipasavyo kwa wananchi.

Diwani huyo alisema hayo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba mapema wiki hii katika kijiji cha Dihombo, kata ya Hembet

i wilayani hapa. Mwigulu alifika kijiji cha Kambara kujionea hali baada ya mifugo 80 wakiwamo mbuzi, kondoo na ndama kukatwa mapanga na wengi kufa na wengine kujeruhiwa.

“Mimi ingawa nipo upinzani lakini ni muumini mkubwa wa falsafa ya Rais Dk Magufuli. Nimekubali kwa asilimia 100 ya uchapakazi wake...na hii inatakiwa ifanyike kwa viongozi wengine wa ngazi ya wilaya hii ya Mvomero tofauti na ilivyo sasa ambapo migogoro ya wakulima na wafugaji bado inaendelea kutokea,” alisema.

Alimtaka Mwigulu kuwa makini na migogoro hiyo kwa kuanza kuchunguza mwenyewe kubaini kiini chake badala ya kusikiliza taarifa za viongozi wa ngazi ya wilaya hiyo, ili afanye maamuzi sahihi ya kumaliza migogoro baina ya wakulima na wafugaji wilayani humo.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.