KAVILA: TUNAHITAJI POINTI TATU KUTOKA KWA SIMBA SC KESHO




Nahodha wa Kagera sugar, George Kavila ameiambia BOIPLUS kuwa wanaiheshimu Simba na ina wachezaji wazuri lakini wanaihitaji kubaki na pointi tatu ambazo zitawaweka mahali pazuri kwenye msimamo wa ligi kwani wamekuwa wakisuasua. 

"Kiukweli tukiifunga Simba hatutalala maana ni mechi ngumu kwetu, tunahitaji ushindi na wao wanataka ushindi ila ninaimani tutashinda, wameshinda mechi nne mfululizo na sisi tumeshinda mbili mfululizo hivyo tunataka kuendeleza ushindi huo," alisema Kavila. 

Kavila alisema kuwa wataingia uwanjani wakiwa wanafahamu mbinu za kocha wa Simba Jackson Mayanja ambaye amewafundisha kwa miaka mingi kabla ya kuachana na timu hiyo. 

"Tuna mbinu mpya za ushindi, tuna kocha mpya ambaye kwa upande wa Simba hawajui vizuri mbinu zake. Tunafahamu Mayanja ni kocha mzuri ila mbinu zake za ushindi tunazijua hivyo tumejipanga kwa ushindi," alisema
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.