JENGO LA HOSTELI CHUO CHA MADINI LAKAMILIKA
Jengo jipya la hosteli ya wasichana la Chuo cha Madini Dodoma (MRI) ambalo ujenzi wake umekamilika hivi karibuni.
Bwalo la wanafunzi wa Chuo cha Madini Dodoma baada ya kukarabatiwa na kupanuliwa.
Mkuu wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa bwalo la wanafunzi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo chaTehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza. Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM Architects Ltd, Peter Matinde.
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika akikabidhiwa funguo za jengo la hosteli la Chuo cha MRI na Mkandarasi aliyejenga jengo hilo kutoka kampuni ya Chichi Engineering Construction Ltd, Shaibu Katindi. Wanaoshuhudia ni Msanifu Majengo wa SMMRP, Arch. Joseph Ringo (kulia), Mkuu wa Chuo cha MRI, Mhandisi Oforo Ngowi (kushoto kwa Mkandarasi), Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na washauri waliosimamia ujenzi wa jengo hilo.
Mkuu wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi (wa pili kutoka kulia) akifafanua jambo wakati wa ukaguzi wa bwalo la wanafunzi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Nishati na Madini, Caroline Musika akifuatiwa na Mkuu wa Kitengo chaTehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza. Wa kwanza kulia ni Mshauri Mwelekezi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PSM Architects Ltd, Peter Matinde.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Chichi Engineering Construction Ltd, Shaibu Katindi (kulia) akielezea jambo kabla ya kuanza kwa ukaguzi wa jengo la hosteli. Wengine katika picha ni wakaguzi pamoja na washauri waliosimamia ujenzi wa jengo hilo.
Msanifu Majengo wa SMMRP, Joseph Ringo (mwenye shati jeupe) akifafanua jambo katika kikao na Mkuu wa Chuo cha Madini cha Dodoma, Mhandisi Oforo Ngowi (mbele katikati) mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama, Wizara ya Nishati na Madini, Francis Fungameza na kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Nishati na Madini, Caroline Musika.