JE MANCHESTER UNITED WALIKUWA SAHIHI KUWAUZA NYOTA HAWA VIJANA?
Kuna baadhi ya majina makubwa sasa katika soka lakini pia kuna baadhi yao wamepata mafanikio makubwa toka walipoondoka Old Trafford ikiwa kwa kuuzwa au kuondoka bure (Free Agent)
Ni idadi kubwa ya nyota wa sasa ambao walipata bahati ya kucheza Manchester United lakini hawakufanikiwa kung’ara kwa namna moja au nyingine na mwisho wa siku waliishia kuoneshwa mlango wa kutokea Old Trafford.
Wachezaji amabao walitimka Old Trafford kwa sababu mbalimbali ni kama;
Robbie Savage
Alijiunga na Crewe mwaka 1994 bure akiwa na umri wa miaka 19
Ni kiungo raia wa Welsh aliyejipatia umaarufu kwa kuchezea vilabu vya Leicester, Birmingham, Blackburn na Derby kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka katika kituo cha televisheni cha BT Sport.
Keith Gillespie
Aliuzwa kwenda Newcastle kwa ada ya pauni milioni 1 akiwa na umri wa miaka 19
Aliuzwa St. James’ Park kama sehemu ya dili lililomfanya Andy Cole kujiunga na Manchester United. Beki huyo wa kulia alienda kujiunga na Newcastle katika kikosi ambacho nusu kichukue ubingwa mwaka 1996.
Giuseppe Rossi
Aliuzwa Villareal mwaka 2007 kwa ada ambayo haiukuwekwa wazi akiwa na umri wa miaka 20
Alikadiriwa kuwa moja ya hazina kubwa Oldt Trafford lakini alifunguliwa mlango wa kuondoka mwaka 2007 baada ya kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara, kuondoka kwa muitaliano huyo kulikuwa sahihi kabisa kutokana na rekodi ya majeruhi ambayo Rossi ameendelea nayo akiwa Villareal pamoja na Fiorentina kwa sasa Rossi yupo kwa mkopo katika klabu ya Levante ya Ligi kuu Hispania.
Ryan Shawcross
Aliuzwa Stoke City mwaka 2008 kwa ada ya pauni milioni 1 akiwa na umri wa miaka 20
Kutokana na kuonesha soka la hali ya juu katika nafasi yake ya beki wa kati Sawcross amekuwa kipoenzi cha mashabiki wa Stoke City pale Britannia Stadium na mpaka kupewa unahodha wa klabu hiyo.
Kwa sasa Shawcross anaweza kusajiliwa tena na Mashetani wekundu kama wakihitaji huduma yake.
Gerard Pique
Aliuzwa Barcelona mwaka 2008 kwa ada ya pauni milioni 3.75 akiwa na umri wa miaka 21
Tangu alipoondoka Old Trafford Pique ameshinda kila kitu kinachotakiwa kushinda katika mchezo wa soka kama vile: Kombe la dunia,Euro,makombe matatu ya ligi ya mabingwa (UEFA),Makombe matano ya La Liga,makombe matatu ya Copa Del Rey,makombe matatu ya Super Cup,na makombe matatu ya klabu bingwa ya dunia kwa sasa thamani yake ni pauni milioni 50, ni moja ya wachezaji amabao Manchester United wangetamani kama wangekuwa naye kwa sasa japokuwa kwa kipindi kile mabeki wa kati walikuwa ni Rio Ferdinand na Nemanja Vidic ilikuwa shida kwa Gerard Pique kutoboa kikosi cha kwanza.
Danny Drinkwater
Aliuzwa Leicester City kwa ada ya pauni laki 6.75 akiwa na umri wa miaka 21
Moja ya nyota wa Leicester City ambao wanapambana kuchukua kombe la ligi kuu ya England msimu huu, na kuna uwezekano wa kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwa mara ya kwanza, Drinkwater ni moja kati ya viungo wenye nguvu na stamina, angeweza kuwa msaada mkubwa kwa sasa United.
Ravel Morrison
Aliuzwa Westham mwaka 2012 kwa ada ya pauni laki 6 kiwa na umri wa miaka18
Moja ya makinda ambao kwa mara ya Kwanza kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson aliwahi kusema kuwa ni “mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu Sijawahi kuona”.
Lakini Morrison amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya nidhamu nje ya uwanja mabyo ikihusishwa zaidi na kutumia vibaya mitandao ya kijamii kama twitter kitu mbacho ameendelea nacho mpaka alivyofika Westham, kwa sasa yupo kwa mkopo Lazio ya Nchini Italia.
Paul Pogba
Alijiunga Juventus akiwa mchezaji huru mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 19
Pogba aliondoka Old Trafford baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza United walikuwa na matatizo ya majeruhi lakini badala ya kumchagua Pogba, Sir Alex Ferguson aliamua kumuingiza Rafael Da Silva katika kiungo na kumuacha Pogba katika benchi kwa muda wote wa dakika 90 katika mchezo ambao United ilipokea kichapo cha goli 3-2 dhidi ya Blackburn Desemba mwaka 2011.
Tangu atimke Old Trafford Pogba amepata mafanikio na kuwa moja ya viungo bora duniani huku akiisaidia Juventus kufika fainali ya UEFA mwaka jana. kwa sasa Pogba ana thamani ya pauni milioni 70.
Wilfred Zaha
Aliuzwa Crystal palace kwa ada ya pauni milioni 3 mwaka 2015 akiwa na umri wa miaka 22
Usajili wa mwisho wa zama za Sir Alex Ferguson, Winga ambaye fomu yake haitabiriki alikumbwa na matatizo mbalimbali nje ya uwanja lakini kubwa zaidi ikiwa ni kiwango kibovu au msimu mbovu ambao Man United ilipitia chini ya David Moyes kiasi cha kocha huyo kushindwa kumuamini kijana na kumpa nafasi ya kuonesha uwezo wake Old Trafford, Zaha alistahili kupewa muda United ili kuonesha kiwango chake kama anachokionesha kwa sasa Crystal Palace.