Jaribio la Rocket la Korea Kaskazini Umoja wa Mataifa walaani vikali




Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeilaani vikali Korea ya Kaskazini kwa kurusha roketi lake la masafa marefu, ambalo viongozi wa dunia wameliita jaribio la hatari la teknolojia ya makombora.

Baraza hilo la Usalama limesema litapitisha azimio lenye vikwazo vipya vikali dhidi ya Korea Kaskazini.

Jaribio hilo la jana lilizikasirisha Japan, Korea Kusini na mshirika wao Marekani, ambao ndio walioitisha kikao cha dharura cha Baraza la Usalama.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power, aliwaambia waandishi wa habari kwamba “Korea Kaskazini haitawachwa tena kujifanyia mambo ipendavyo.”

Korea Kaskazini inasema ilirusha roketi hilo kupeleka kifaa cha uchunguzi angani, ikiwa ni mwezi mmoja tu baada ya kufanya jaribio lake la nyuklia.

Marekani inahofiwa kuwa huenda ikaharakisha mpango wake wa kuweka mitambo ya silaha kwenye rasi hiyo, kufuatia jaribio hilo la Korea Kaskazini.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.