FELLA AFUNGUKA HAYA KUHUSU JUMA NATURE
Diwani wa Kilungule kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Said Fella, ambaye pia ni meneja wa kikundi cha Mkumbwa na wanawe,Wanaume Family na nyota wa mziki wa Bongo Diamond Platnumz, amefunguka na kusema kuwa Juma Nature ndiye msanii aliyemshawishi kujihusisha na masuala ya muziki.
Hii imeibua ukweli uliofichika ambapo wengi walikuwa wanafahamu kuwa Juma Nature alikua chini ya Management ya Fella jambo ambalo sio la kweli kwani Nature ndiye alikuwa na mchango mkubwa kwa Fella kwenye kuujua muziki wa Bongo.