Zito: Nimeridhika Utekelezaji Elimu Bure

imbo la Kigoma Mjini, Kabwe Zitto amefanya ziara katika shule ya msingi Kigoma iliyopo katika Manispaa ya Kigoma Ujiji ambako alipata elimu yake ya msingi na kuahidi kuifanyia matengenezo makubwa kutokana na hali mbaya ya uchakavu wa miundombinu na madarasa. Zitto alikuwa kwenye ziara ya kuona utekelezaji wa mpango wa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari uliotangazwa na serikali na namna fedha zilizoahidiwa na serikali zilivyopokewa shuleni na changamoto zilizopo.
Akiwa shuleni hapo ambako alipata elimu yake ya msingi kati ya mwaka 1984 hadi mwaka 1990, Zitto alionesha kusikitishwa na hali mbaya ya majengo ya shule hiyo, upungufu mkubwa wa madawati huku shule hiyo ikiwa haina uzio na kufanya kuwa na mwingiliano mkubwa baina ya wanafunzi na wapita njia.
Katika kufikia tamati ya nini wafanye kuhusu shule hiyo, mbunge huyo kupitia Chama cha ACT-Wazalendo ambaye aliongozana na Diwani wa Kata ya Kigoma Mjini, Hussein Kalyango ambaye pia amesoma shuleni hapo, alisema wataitisha harambee kubwa ambayo sehemu kubwa itajumuisha watu waliosoma shuleni hapo.
“Wapo watu wengi ambao walipitia shuleni hapo ikiwemo familia ya mmiliki wa mabasi ya Saratoga ambao tutawasiliana na kupanga namna ya kupata fedha za kutosha kuifanyia ukarabati mkubwa shule hii ambayo ni moja ya shule zenye umaarufu mkubwa nchini, zamani ikijulikana kama Aga Khan Kigoma Primary School,” alisema Zitto.
Awali katika taarifa yao kwa mbunge huyo, walimu walisema kuwa ina hali mbaya ya miundombinu na madarasa matatu hayatumiki kutokana na kubomoka baada ya msingi wake kuathiriwa na mvua.
Mmoja wa walimu hao, Richard Katunka alisema, shule haina uzio hivyo wapita njia wamekuwa wakitumia vyoo sambamba na wanafunzi huku tatizo la wizi wa vitu mbalimbali likichangiwa na kutokuwa na uzio huo.
Akielezea ziara yake ya kuona utekelezaji wa elimu bure, Zitto alisema ameridhishwa na namna serikali inavyotekeleza mpango huo ambao utatoa nafuu kwa wazazi katika kusimamia elimu kwa watoto wao.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.