Watu 62 wanamiliki nusu ya utajiri wa dunia
Matajiri
zaidi 62 duniani, hivi sasa wanamiliki zaidi ya nusu ya utajiri wa
wakaazi wote wa dunia, limesema shirika la hisani la Oxfam, kuelekea
mkutano wa kiuchumi wa dunia - World Economi Forum (WEF) Davos, Uswis.
Ripoti
hiyo ya Oxfam inasema utajiri wa watu hao 62 matajiri zaidi umeongezeka
kwa asilimia 44 tangu mwaka 2010, huku utajiri wa watu maskini zaidi
bilioni 3.5 umeshuka kwa asilimia 41. Ripoti hiyo iliyopewa kichwa cha
habari kisemacho: "Uchumi wa asilimia 1", inabainisha kuwa wanawake
wanaathirika zaidi na ukosefu wa usawa duniani.
Karibu
nusu ya matajiri zaidi wa dunia wanatokea nchini Marekani, 17 barani
Ulaya na waliosalia wanatoka katika mataifa yakiwemo China, Brazil,
Mexico, Japan na Saudi Arabia.
Moja ya
mambo muhimu yaliyoainishwa katika ripoti ya Oxfam ambayo yanayochangia
ukosefu wa usawa duniani ni kupungua kwa mgao wa pato la taifa
linalokwenda kwa wafanyakazi karibu katika mataifa yote yalioendelea na
yanayoendelea, na kuongeza kuwa wengi wa wafanyakazi wanaolipwa kiasi
kidogo zaidi cha mshahara ni wanawake.
Pengo la walio na wasio nacho lazidi kupanuka.(P.T)
Ingawa
viongozi wa dunia wamezidi kuzungumzia haja ya kukabiliana na ukosefu wa
usawa, Oxfam inasema pengo kati ya matajiri zaidi na wengine limetanuka
zaidi katika kipidi cha miezi 12 iliyopita.
Utabiri
wa Oxfam, yaliyotolewa siku moja kuelekea mkutano wa Davos wa mwaka jana
- kwamba asilimia moja ya matajiri zaidi wa dunia watamiliki zaidi ya
sisi sote tuliobakia katika muda usiyo mrefu, ulitimia mwaka 2015,
imeongeza ripoti hiyo.
Wakati
idadi ya watu wanaoishi katika hali ya umaskini uliyokithiri ilipingua
kwa nusu kati ya mwaka 1990 na 2010, wastani wa kipato cha asilimia 10
ya watu maskini zaidi duniani umeongezeka kwa chini ya dola tatu kwa
mwaka katika kipindi cha robo karne iliyopita, hili likiwa ongezeko la
chini ya senti moja katika kipato cha mtu mmoja mmoja kwa mwaka.
Zaidi ya
wakuu 40 wa nchi na serikali watahudghuria mkutano wa Davos unaoanza
Jumanne jioni na kumalizika Januari 23. Taarifa ya awali iliyotolewa na
waandaji wa mkutano huo wa uchumi duniani, ilisema mkutano huo wa ngazi
ya juu unaofanyika katika eneo la mapumziko la Davos nchini Uswisi
watahusisha pia viongozi wapatao 2,500 wa kibiashara na kijamii.
Mapinduzi ya nne ya kiviwanda
Akifafanua
kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu -- Mapinduzi ya nne ya kiviwanda --
mwasisi wa WEF Klaus Schwab amesema inamaanisha kuunganisha teknolojia
katika ulimwengu wa kimaumbile, kidigitali na kibayolojia, ambako
kunaanzisha uwezo mpya kabisaa na kuathiri mifumo ya kisiasa, kijamii na
kiuchumi.
Mkurugenzi
mkuu wa shirika la Oxfam Winnie Byanyima, ambaye anahudhuria mkutano wa
Davos baada ya kuwa mwenyekiti mwenza wa mkutano wa mwaka uliyopita,
alisema haikubaliki kwa nusu ya watu maskini zaidi wa dunia kumiliki
siyo zaidi ya matajiri zaidi wachache, ambao wanaweza kuingia katika
basi moja.
Utajiri wa Afrika nje
Kama
kipaumbele, Oxfam inataka kukomeshwa kwa enzi ya maeneo salama ya kodi,
ambao yameshuhudia ongezeko la matumizi ya vituo vya nje kukwepa kulipa
kodi. "Hili linazinyima serikali rasilimali muhimu zinahitajika
kupambana na umaskini na ukosefu wa usawa," inasema ripoti hiyo.
Karibu
asimilia 30 ya utajiri wa kifedha wa Afrika unakadiriwa kushikiliwa nje
ya bara hilo, iliongeza ripoti hiyo, na hivyo kugharimu takribani dola
bilioni 14 katika mapato yanayopotezwa kila mwaka.
Kufikia
viwango sahihi vya kodi kutakuwa muhimu ikiwa viongozi wa dunia
watafikia malengo yao, waliojiwekea mwaka uliyopita, ya kufuta kabisaa
umaskini uliyokithiri ifikapo mwaka 2030.
Byanyima
aliwapa changamoto washiriki wa mkutano wa Davos kutoa mchango wao
katika kukomesha enzi ya maeneo salama ya kodi, ambayo yanachochea
ukosefu wa usawa wa kiuchumi na kuwazuwia mamia ya mamilioni ya watu
kujiondoa katika umaskini.
Miongoni
mwa watu 62 wanaosemekana kumiliki utajiri sawa na asilimia 50 ya
maskini zaii, Oxfam ilisema 53 ni wanaume na tisa tu ndiyo wanawake, hii
ikionyesha kuwa hata kwenye ngazi za juu wanawake wanawakilishwa
vibaya.
Chanzo:DW