The site for daily Tanzania Hard News and Entertainment
Home/Udaku/Wanawake Wengi Hufikiri Kuwa Wanaume Wote Wanatabia Hizi.
Wanawake Wengi Hufikiri Kuwa Wanaume Wote Wanatabia Hizi.
Hakuna
maana moja ya kumuelezea mwanaume, ila kwa aliye mwanaume nadhani
anaelewa nini maana ya kuitwa mwanaume, mara nyingi wanawake huwa
wanaonekana wao ndio wanaonewa sana na wanaume na ni vigumu sana kujua
manyanyaso ya wanaume sababu wengi huwa hawayaongelei, wanawake wengi
huwaongelea wanaume kwa ujumla yaani kuwafananisha wote katika kundi
moja. lakini kuna mtu na mtu kila mtu ana tabia zake na wanaume wana
tofautiana, sina maana ya kutetea haki za wanaume ila kuna fikira
potofu kuhusu wanaume ambazo watu wanatakiwa kuzitoa akilini.
Mwanaume halii.
Mwanaume
akionekana analia ataitwa dhaifu, ama hajakuwa bado mtoto, lakini
ukweli ni kwamba hata wanaume wana hisia wana umia na wana mioyo kama
wanawake, wao sio maroboti japokuwa inachukuliwa kuwa mwanaume
anayaeweza kuvumilia maumivu ndio jasiri bila kujua sio kila anaye lia
kwa machozi ni mnyonge. Kuna usemi wa mwandishi Malorie Blackman alisema
“Boys don’t cry, but men do.” katika kitabu chake cha Boys Don’t Cry.
Wanaume Wakorofi.
Wapo
wanawake wengi wameumizwa na vitendo vya kikatili kutoka kwa wanaume
zao, ndugu zao na marafiki, kupigwa na kuteswa na wanaume zao, lakini si
kweli wanaume wote wakorofi na wanadharau wanawake au watoto, wapo
wanaume wanaojali na kuheshimu wanawake pia.kuna mtu alisema ukitaka
kujua mwanaume mwenye hekima tazama heshima yake na mapenzi yake kwa
mama yake.
Wanaume hawafanyi Kazi za Nyumbani.
Kazi
za nyumbani sikuzote huonekana ni za wanawake tu,ni mara chache usikie
baba anaandaa chakula kwa ajili ya familia yake hata kama baba huyo
amesomea Mapishi na ana Degree, lakini wapo wanaume wanaosaidia
wake/wapenzi wao wakiwa nyumbani, kama ni kufua kupika na kuosha vyombo
wapo wanaojua nini maana ya kusaidia kazi za nyumbani.
Mwanaume ndiye Anaepanga Maamuzi juu ya Mwanamke.
Sikataii
wapo wanaume wa aina hii, wao wanapanga kila kitu, yeye ndo atakwambia
fanya hivi na usifanye hivi kitu ambacho si kila mwanaume anafanya,
wapo wanaojali maamuzi ya wenza wao na kuheshimu mambo yao, tusiishi kwa
mazoea.
Wanaume Wanapenda Michezo.
Hapa
sanasana mpira wa miguu, nilishangaa siku moja nilimuuliza mshikaji
mmoja anapenda timu gani ya mpira wa miguu alinijibu kirahisi tu ye si
mpenzi wa mpira wa mguu , nilishangaa lakini ukweli wapo wanaume ambao
sio wapenzi wa mpira wa miguu, ni kawaida kukutana na watu tofauti.