UMEIPTA HII: Mkuu wa Shule Huko Njombe Agoma Kupokea Viporo vya Ada, Kwa Hofu Ya Magufuli
MKUU wa Shule ya Sekondari ya Viziwi Njombe wilaya ya Njombe mkoani
Njombe, Alex Chengula, amegoma kupokea fedha za viporo vya ada za
wanafunzi za mwaka uliopita.
Aligoma kupokea fedha hizo, akiogopa kwenda kinyume na agizo la serikali, linalokataza wakuu wa shule za msingi na sekondari kutoza michango kwa wanafunzi.
Tukio hilo ni la Jumamosi ya wiki iliyopita katika mkutano wa wazazi na uongozi wa shule. Shule hiyo hufanya mikutano hiyo kila mwaka kupokea taarifa za maendeleo ya shule kila mwanzo wa mwaka.
Katika kikao hicho, mkuu huyo aliwaarifu mabadiliko yaliyofanywa na serikali kuhusu uchangiaji elimu kwamba kuanzia mwaka huu elimu ni bure.
Alisema, shule yake imepokea waraka kutoka serikalini unaowataka walimu kutochangisha michango yoyote shuleni, badala yake serikali itagharamia uendeshaji wa shule.
Mkuu huyo wa shule aliwaarifu wazazi kuwa kabla ya kupokea waraka wa serikali juu ya zuio la kukusanya ada na michango hiyo, tayari uongozi wa shule umewapelekea wazazi taarifa ya kiasi cha ada wanachostahili kulipa mwaka huu na madeni kwa wale ambao hawakamilisha malipo ya ada na michango hiyo mwaka jana.
Alisema alishaarifiwa na baadhi ya wazazi kuwa walishalipa fedha hizo kupitia akaunti ya shule na hivi sasa uongozi wake, unawasiliana na wazazi hao ili shule iwarejeshee fedha hizo.
Kufuatia serikali kufuta ada na michango, shule yake imejikuta inadaiwa zaidi ya Sh milioni tano kutokana na kukopa vifaa vya maabara na kemikali na malipo ya walimu waliosalia shuleni kuwafundisha wanafunzi, wanaojiandaa kwa mitihani ya kitaifa.
Kuhusu kuwalipa walimu posho ya kazi kwa muda wa ziada, mwalimu huyo alifafanua kuwa wanafunzi viziwi kwa kawaida wakikaa japo mwezi mmoja bila kufundishwa, hupoteza kumbukumbu.
Alisema kila mwaka walimu kuwafundisha wanafunzi wakati wa likizo ili kuwaweka tayari kwa mitihani na walimu hao hulipwa shule zikifunguliwa Januari.