UMEIPATA HII>>>Mawaziri CUF Waenguliwa Uzinduzi wa Miradi Zanzibar

 
 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeamua kuwaengua mawaziri kutoka Chama cha Wananchi CUF katika ratiba ya uzinduzi wa miradi ya Maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi kufuatia msimamo wao wa kutoitambua serikali ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein.
 
Kwa mujibu wa ratiba ya sherehe hizo iliyotolewa jana mjini Zanzibar na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, serikali imeamua miradi yote kuzinduliwa na mawaziri kutoka chama tawala cha CCM, wakiongozwa na Rais Dk. Shein.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.