UKAWA WASUSIA UCHAGUZI WA KAMATI ZA BUNGE
Chama cha
Mapinduzi (CCM) kimefanikiwa kuchukua nafasi nyingi za wenyeviti na
makamu wake baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa kamati Bunge
katika uchaguzi uliofanyika leo.
Hawa
ndio wenyeviti na makamu wake katika kamati hizo, Kamati ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC) Mwenyekiti atatoka vyama vya upinzani ambapo
bado hajafahamika ila Makamu wake ni mbunge wa Mwibara Kangi Lugola
(CCM).
Waliochaguliwa
katika kamati nyingine ni pamoja na mbunge wa Kigoma Kaskazini Peter
Serukamba (CCM) ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Huduma na Maendeleo ya
Jamii, na Makamu wa wake ni Mbunge wa Busega Raphaeli Chegeni (CCM).
Kamati
ya Sheria ndogo itaongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge
(CCM) na makamu wake ni mbunge wa Sengerema William Ngeleja (CCM)
Kamati
ya Nishati na Madini mwenyekiti ni mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa
Singida Martha Mlata na makamu wake ni mbunge jimbo la Chumbuni Ussi
Pondeza (CCM).
Kwa
mujibu wa kanuni za Bunge mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali
(PAC) anatakiwa kutoka upinzani hivyo bado hajachaguliwa. Kwa upande wa
makamu wake aliyechaguliwa ni mbunge wa Sumbawanga Mjini Aeshi K.
Hilary (CCM).
Wakati
uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge ukifanyika taarifa
zilizotufikia katika mtandao huu ni kwamba Wabunge wote wa Upinzani
wamegoma kushiriki katika uchaguzi huo kwa madai kuwa umefanywa bila
kuzingatia masuala muhimu.