Tukumbushane; Julius Aghahowa Kwenye World Cup 2002



Ndugu zangu,
Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2002 ziling'arishwa na ujio wa kijana Julius Aghahowa na staili yake ya kushangilia magoli kwa kupiga samasault za kinyumenyume.
Na rekodi ya Julius Aghahowa ni kwenye mechi dhidi ya Sweden. Julius Aghahowa alifunga bao zuri na alishangilia kwa kupiga samasault saba za kinyumenyume huku akiwa amekunja miguu kwa mikono yake. Hiyo ni rekodi ambayo haijavunjwa hadi hii leo.
Bao la Julius Aghahowa halikutosha kuivusha Nigeria kwenye hatua ya makundi. Henke Larsson alijibu kwa kufunga mabao mawili, moja la kichwa baada ya mpira wa kona , na la penalti.
Tutamkumbuka Julius Aghahowa kwa kutuletea wapenzi wa soka burudani ile...
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.