TANESCO Yakanusha Kuuza Asilimia 49 ya Hisa Zake
Tunakanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Citizen la Januari 5, 2016 katika ukurasa wake wa 12 yenye kichwa cha habari: ‘Umma kununua asilimia 49 ya hisa za Tanesco’. Mwandishi na Mhariri wamejiandikia taarifa hiyo kwa sababu wanazozijua wao.
Sehemu ya taarifa inasema: Serikali ya Tanzania ina mpango
wa kuuza hisa ya Shirika la Umeme Tanzania kwa umma...
Pia, sehemu nyingine inasema: Waziri
wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo aliliambia gazeti la East African
kuwa Serikali itatoa asilimia 49 ya hisa za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
wakati huo Serikali ikibaki na hisa zingine...
