SERIKALI YAKANUSHA UZUSHI UNAOENEZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUMHUSU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Kaimu
Mkurugenzi wa idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akitoa
ufafanuzi juu ya taarifa za uzushi unaosambazwa katika mitandao ya
Kijamii ya ndani na nje ya nchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimwa Dkt. John Pombe Magufuli amefukuza wageni kutoka nje
waliokuwa wanafanya biashara hapa nchini kwa kuwa Serikali yake
haitataki wageni wafanye bishara zao nchini ambapo ukweli ni kwamba
Serikali haijafukuza wageni wanaofanya biashara zao nchini na haina
mpango wa kufanya hivyo kwa wageni wanaoishi nchini kwa vibali
vilivyotolewa kisheria na Serikali.kushoto ni Naibu Kamishna na Msemaji
wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya na mwisho kushoto ni Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Ndani Isaac Nantanga,Kulia ni Naibu Kamishna wa
Idara hiyo Bw.Wilson Bambaganya.