Ole Sendeka Amjibu Dk Makongoro Mahanga ....Asema Makatibu Wakuu na Manaibu wao Sio Wajumbe Wa Baraza La Mawaziri
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na mbunge wa zamani wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka amewataka watanzania kuwa makini na kuzipuuza kauli zinazoenezwa na baadhi ya watu kwenye mitandao kuwa serikali ya Dk John Magufuli imekuwa na baraza kubwa la mawaziri kuliko alivyo ahidi na kwamba serikali inaweza kuwa nagharama zaidi kwakuwa kauli hizo zinalengo la kufifisha juhudi za serikali ya awamu ya tano kufanya mabadiliko ya kiuchumi kwa watanzania.