NI VEMA UKAYAJUA HAYA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA:

1. Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa ni
ya maisha yote.
2. Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka
kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada ya
Ndoa.
3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.
4. Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu
yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi
fanywa na mtu yeyote.
5. Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na
Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.
6. Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama kuolewa na
mtu hasiye sahihi.
7. Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
a) Walevi. b) Malaya. c)Wagomvi.
8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe na
Ndoa yenye furaha.
9. Maneno matatu yanayojenga amani katika Ndoa:
a) Nakupenda. b) Samahani. c) Asante.
10. Kupiga punyeto ni kujiharibu.
11. Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama anga bila
jua.
12. Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu:
Mungu mmoja - Mume mmoja - Mke mmoja.
13. Furaha ya kudumu maisha hutegemea na chaguo
lako la Ndoa.
14. Usioe pesa au mali - muoe mtu.
15. Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa
isiyo na amani na furaha.
16. Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano
mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke mbaya,
bali anahitaji kupendezeshwa.
17. Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama kuolewa na
mwanamume/mwanamke kwa kigezo tu anakidhi
haja zako kingono.
18. Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki wema.
19. Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali.
20. Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.