Mbunge ‘awainua’ bodaboda
MBUNGE wa jimbo la Nachingwea, Hasani Masala ametoa pikipiki tatu zenye thamani ya Sh milioni sita na fedha taslimu Sh 500,000 kwa Umoja wa madereva wa bodaboda wilayani hapa, huku akiwataka kusajili umoja huo ili utambulike kisheria.
Mchango huo ameutoa alipokutana na madereva wa bodaboda juzi ambapo licha ya kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo, aliwaasa kuunda umoja wenye nguvu
na kuwa na mfuko wa kuweka na kukopa ili uwasaidie katika kuwapatia mitaji.
Aliwataka viongozi wa umoja huo kuwatambua madereva wote wa bodaboda wilayani na kwa kupitia vituo vyao vya kazi maarufu migundi kuunda uongozi ambao ndio utakuwa ndio wawakilishi, hivyo kurahisisha mawasiliano kati ya uongozi na taasisi mbalimbali ikiwemo kikosi cha usalama barabarani.
Masala alisema msaada wa pikipiki alizowapatia ni mtaji katika kuanzisha Vicoba endelevu ambapo ndio patakuwa kimbilio kwa madereva hao ili kuachana na kutumwa, badala yake waweze kumiliki pikipiki zao wenyewe kwa kukopeshana wenyewe kupitia mfuko huo.
“Mimi nipo nyuma yenu katika kuhakikisha mnafanikiwa kuunda mfuko wa Vicoba endelevu ambacho ndicho chombo pekee kitakachokuwa mkombozi wenu,” alisema Masala.