Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya kutumia lugha ya matusi kwa maofisa wa Jeshi la Polisi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Lawrence Masha (45) ambaye kwa sasa ni kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).