Makaburi ya pamoja 'yagunduliwa' Burundi
Image copyrightImage captionPicha moja ya satelaiti ambayo shirika la Amnesty linasema inaonyesha kuwepo kwa kaburi la pamoja
Shirika la Amnesty International limesema limepata picha za satelaiti zinazoonyesha uwepo wa makaburi matano ya pamoja katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura.
Maafisa wa usalama wanadaiwa kuua watu wengi baada ya kuenea kwa machafuko mwezi Desemba.
Amnesty limesema picha hizo zinaonyesha makaburi hayo yaliyozikwa watu wengi kwa pamoja eneo la Buringa viungani mwa Bujumbura.
Shirika hilo limesema uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouwawa siku ya tarehe 11 Desemba, siku ambayo ilishuhudia machafuko makubwa mjini Bujumbura.
Watu zaidi ya 87 waliuawa wakati wa msako uliofanywa na maafisa wa usalama Desemba, baada ya kambi za jeshi kuvamiwa na watu wenye silaha.
Umoja wa Mataifa umesema idadi halisi huenda ikawa juu.
Umoja huo umesema pia unatathmini picha za satelaiti kuchunguza ripoti za kuwepo kwa mataburi tisa ya pamoja, moja katika kambi ya jeshi ambalo linakadiriwa kuwa na miili zaidi ya 100.