HAWA NDIYO MAADUI WAKUBWA WA DIAMOND
Staa wa ngoma ya Utanipenda, Nasbu Abdul ‘Diamond’.
…’nayosema
yana maana, sababu hakuna anayejua kesho, anayepanga ni Rabana, ila
ameificha ni confidential, ukisali omba sana, mumeo nisije kuwa
kichekesho, Maana rafiki wa jana, ndiye adui mkubwa keshoo!!!”
Ni
mojawapo ya verse (ubeti) uliyomo kwenye hit single ya staa wa Bongo
Fleva, Nasibu Abdul ’Diamond’ iitwayo Utanipenda? Wimbo ambao ndani ya
takriban siku 30 tangu kuachiwa kwa video yake kwenye Mtandao wa YouTube
umetizamwa karibu mara milioni 2!
Katika wimbo huo, Diamond amejaribu kuvuta hisia na kujiweka katika nafasi ya msanii maarufu atakayefulia siku moja.
Amejaribu kuvuta picha na namna ambavyo mambo yanavyoweza kutokea kwake binafsi na kwa familia yake.
Ameenda
mbele zaidi kuwazungumzia wadau wake wakubwa, au ‘marafiki zake’ katika
mafanikio yake ya sasa namna ambavyo wanaweza kumgeuka, kwa sababu
anatambua kwamba ‘rafiki wa jana, ndiye adui mkubwa kesho’
Katika
Showbiz ya leo, nakuletea listi kamili ya ‘marafiki’ hao wanaoweza kuja
kuwa ‘maadui wakubwa’ kesho ambao amewataja kwa majina mmojammoja na
nguvu au mchango walionao katika maisha yake ya sasa na ya baadaye, japo
hatuombei wala hatutarajii yamkute aliyoyawaza, lakini kama alivyosema
mwenywewe ‘ Anayepanga ni Rabana, ila ameificha (kesho), ni
confidential;
MENEJA TALE
Ametajwa
kwenye vesi ya kwanza tu ya wimbo huo. Anajulikana kama, Hamis Tale
‘Babu Tale’ au Meneja Tale. Unaweza kusema ndiye Meneja Mkuu wa Diamond
Platnumz.
Ni
miongoni mwa wadau wakubwa vijana wa muziki nchini Tanzania, anasimamia
na kuratibu karibu shoo zote za msanii huyu, ndani na nje ya Tanzania.
Ndiye anayepokea michongo yote ya shoo za Daimond na kundi zima la
Wasafi Classic Baby (WCB).
Katika
wimbo huo, Diamond amemuweka katika kundi la meneja ambaye mambo
yakiharibika, atakuwa hamtaki tena kiasi kwamba hata akimuona kwa mbali,
atakuwa ana lala mbele (anamkimbia ni sheedah! Ameimba; Redio nyimbo
wamezima, TV ndiyo hatari, meneja umebaki jina, hanitaki hata Tale…).
KIMWANA
Huyu
ni dada wa hiyari wa Diamond, anajulikana zaidi kwa majina ya Halima
Kimwana, ambaye amekuwa mtu wa karibu sana wa msanii huyo kiasi cha
wengine kusema ni mpenzi wake ama dada yake damdam. Kutokana na ukaribu
huo, bila shaka anajua mambo mengi ya Diamond na anaweza kuwa na athari
katika maisha yake.
Kimwana
ametajwa katika wimbo wa Utanipenda katika mstari mmoja wapo, pale
Diamond anaposema “Kimwana sidadaangu, eti naye hanifahamu…” akimaanisha
kwamba siku atakapofulia, Kimwana atajifanya hamfahamu licha ya ukaribu
walionao sasa!
HARMONIZE
Ni
msanii chipukizi anayetamba na ‘hit singo’ ya Aiyola, majina yake ya
kwenye paspoti ni Rajabu Abdulkhali a.k.a Harmonize. Kama Harmonize ana
mtu anayemheshimu na kumthamini sana katika mafanikio aliyoyapata hadi
sasa, basi ni Diamond, kwani ndiye msanii aliyetambua kipaji chake na
kuamua kumsaidia kwa kumuweka chini ya lebo yake (WCB) na kuwa msanii wa
kwanza kutolewa na kujulikana ndani ya muda mfupi.
Katika mabadiliko ya kimaisha anayoyatabiri Diamond katika Utanipenda, amemtaja msanii huyu kwa kusema;
“..Hata
Harmonize nikimpigia ananifokea kama Sallam…..” akimaanisha kwamba hata
huyu dogo atasahau wema wote aliomtendea mpaka kufanikiwa na kuanza
kumletea nyodo kiasi cha kumfokea pale anapopigiwa simu ili
amsaidie..dah!
SALLAM
Ni
meneja wa Diamond akishirikiana na Babu Tale. Anajulikana kwa majina ya
Sallam Sharaff ambaye ni mfanyabiashara, promota wa wasanii na mtendaji
mkuu wa SK Entertainment. Ni kijana ambaye anamuongoza na kuendesha
mambo mengi ya Diamond na ndiyo maana kwenye wimbo wake anamwambia
Harmonise atakuwa akimfokea kama Sallam, kwani sasa hivi ndiye kama bosi
wake pia.
JK
Ni
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete, ambaye Diamond anamuelezea kama ni mtu mwenye mchango mkubwa
katika mafanikio yake, mbali ya kuwa ni kiongozi wa nchi, lakini kwake
amekuwa mshauri na rafiki.
Hivyo
katika hali ya kawaida, iwapo ikitokea Diamond akakwama, JK atakuwa mtu
wa kwanza kumkimbilia kuomba msaada,lakini anaweza pia akajikuta
anaishia getini na kufukuzwa.
Kwenye
Video ya Wimbo wa Utanipenda, Diamond amemuonesha mama yake (Sandra)
akiwa amembeba mgongoni mwanaye, Tiffah akienda kwa Jakaya kuomba msaada
lakini anakataliwa na mlinzi hata kuingia ndani, anaishia getini.
FELLA
Jina
lake kamili ni Said Fella, a.k.a Mkubwa Fella, ambaye hivi karibuni
ameukwaa Udiwani wa Kata ya Mbagala jijini Dar es Salaam kupitia Chama
Cha Mapinduzi (CCM). Ni Meneja wa Yamoto Band, mvumbuaji na muendelezaji
wa vipaji vya wasanii wa Bongo hasa vijana, ana kituo cha kuendeleza
vipaji vya muziki wilayani Temeke.
Fella, Tale na Diamond wana masilahi ya pamoja katika Yamoto Band.
Fella
naye ana ‘play part’ kubwa ya mafanikio ya Diamond na ndiyo maana
ametajwa katika wimbo huo kuwa naye anaweza kuja kumgeuka baada ya
kufulia ambapo mama yake anaonekana kweye video akienda kuomba msaada
nyumbani kwa Mkubwa Fella lakini naye anaishia getini.
ROHO YAKE (TIFFAH)
Katika wimbo huu, Diamond anamtaja mtoto wake pekee, Princess Tiffah kama ndiye roho yake iwapo mambo yataharibika.
Diamond
anatuonesha namna ambavyo binti yake atahangaika. Tiffah ndiye mtoto
wake wa kwanza na wa pekee hadi sasa, kwani tangu aanze uhusiano wa
kimapenzi miaka kadhaa iliyopita na wanawake kadhaa, hakuwahi kupata
mtoto.
ZARI
Diamond
ndiye ameshafulia, usupastaa hakuna tena, hapati shoo tena kama zamani
na hata akipata hazijazi watu, kwake ni mikosi tu, sawa na jahazi
kuzama. Swali linakwenda kwa mpenzi wake wa sasa, ambaye ni matawi ya
juu na bila shaka amempenda
Diamond
na kuamua kumzalia mtoto si kwa sababu ya pesa zake, bali pengine kwa
umaarufu wake, kwa sababu ukilinganisha utajiri wa Diamond na wa Zari
unaonesha Zari ni zaidi.
Katika
wimbo huu, Diamond anamtupia swali mama watoto wake; Je, nawe
utanipendaga au nawe ndiyo utanimwaga? (pindi atakapofulia).
MAADUI WENGINE
‘Maadui’
wengine watarajiwa wa Diamond ambao amewatajani pamoja na mashabiki
zake, vyombo vya habari kama redio, TV na magazeti, amekwenda mbele
zaidi kwa kuonesha ni magazeti gani ambayo atakapofulia na kumwagwa na
Zari hayatasita kumuandika.
Kwenye
video yake amelionesha gazeti hili la Ijumaa, gazeti namba moja la
kuandika habari za mastaa nchini Tanzania, kuwa litakuwa na habari zake
ukurasa wa mbele.
ANAUPENDA SANA
Kwa
mujibu wa Diamond mwenyewe, wimbo huu wa Utanipenda ni wimbo ambao
ametokea kuupenda zaidi kuliko nyimbo zake zingine kwa mwaka huu.
Sehemu
au vesi anayoipenda zaidi ni hii inayosema: “…ooo bado nimewaza sana,
zile tunzo, mashauzi ya airport, je itakapofika tamati, utadiriki hata
japo kunipost?
Pindi shows zimekwama, nikipata sijazi ni mikosi, ooh jahazi limezama, Mola ninusuru baba.
“Kama
namuona mwanangu, roho yangu, Tiffah Dangote, Anakwenda na Mama’ngu kwa
Jakaya Kikwete wanafukuzwa watoke, usilie Sandra wangu, mboni yangu,
jikaze usichoke….”
Nadiriki
kusema Utanipenda ni miongoni mwa nyimbo zinazofundisha jamii na
umewasilisha ipasavyo dhima ya msanii kwa jamii. Ni vyema kujua kuna
maisha mengine kesho ambayo hatuyajui na tunatakiwa kujitambua katika
hilo kadiri tunavyopata mafanikio.