Future kuanzisha vita na Ciara? Amshambulia kwenye hizi tweets tano!
Imepita mwaka mmoja na nusu toka Ciara na Future wamkaribishe duniani mtoto wao wa kiume ‘babyfuture’ lakini pengine mwaka huu wa 2016 unaweza kuwa mwaka mgumu kwa staa wa muziki wa R&B, Ciara!
Baada ya ukimya juu ya mvutano unaohusiana na mtoto wao, Future ameonekana kuchoshwa na mambo hayo na hivyo kumwambia Ciara ajiandee kwani visa anavyomuwekea ili kuonana mwanae vimefika mwisho!
Kupitia page yake ya Twitter, Future amefunguka na kuandika tweets hizi tano…
>>> “ Huyu b**** ana matatizo… “ <<< @1future.
>>> “ Inabidi nipitie kwa wanasheria ili kumuona babyfuture… ushenzi wa kulipa dolla 15,000 kwa mwezi ” <<< @1future.