The site for daily Tanzania Hard News and Entertainment
Home/Events/News/ Bandarini si Wizi Bali Kufuru: Meli Nzima 'Yaibiwa'
Bandarini si Wizi Bali Kufuru: Meli Nzima 'Yaibiwa'
Makubwa yamezidi kugundulika kwenye sakata
la upotevu wa makontena Bandari ya Dar na sasa inadaiwa kuwa kuna
nyakati wahusika wamewahi kufuta kumbukumbu za meli nzima ya makontena
na kuiba makontena yote.
Taarifa hizo zinavuja wakati kukiwa na mvutano kati ya chama cha
Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) kinachodai kutohusika kwa namna
yoyote na upotevu wa makontena zaidi ya 11,000 ambayo hayakulipiwa
ushuru bandarini (Wharfage charges).
TAFFA wanaitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuwajibika katika
upotevu huo ulioinyima Serikali kupitia mamlaka hiyo mabilioni ya fedha.