Baada ya kumfukuza Kerr, mipango ya Simba haijaishia kwa Mayanja, wanamtaka kocha huyu …
Baada ya uongozi wa klabu ya Simba kutangaza kumfukuza kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo muingereza Dylan Kerr na kocha wa makipa Iddi, January 18 makumu wa Rais wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu ametangaza ni kweli wapo katika mchakato wa kuongeza nguvu katika benchi la ufundi kwa kumuongeza kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Morocco.
Kaburu amethibitisha kuwa Morocco atakuwepo kama kocha na mshauri wa timu ya Simba kwa kipindi hiki inachofundishwa na kocha mganda Jackson Mayanja, ila hawajaitangaza sana kwa sababu bado mambo hayajakaa vizuri na hawawezi kuweka mambo ambayo bado hayajakamilika.
“Jambo
hilo ni kweli lakini bado hatujaliweka nje kwa maana ya kulijadili,
kwani mambo bado, ni kweli tunamuhitaji Morocco ambaye pia ni muajiriwa
wa TFF, ila wakati huu ambao tupo kwenye mchakato wa kutafuta kocha
mkuu, tuliona kwamba kuna haja ya kuongeza nguvu katika benchi letu la
ufundi” >>> Geofrey Nyange
Kwa upande wa Hemed Morocco amethibitisha kuwepo mpango huo, ambao kwa upande wake amesema kuwa mpango ulianzia Zanzibar
lakini leo January 18 alikuwa asaini mkataba sema kipengele cha
mshahara kilikuwa tofauti na walivyokubaliana awali hivyo anawapa muda
wafikirie.
“Suala
hilo ni kweli lakini naona kama bado hatujaafikiana, suala la upande wa
maslahi kwani tulikuwa hatua za mwisho lakini suala la mshahara
likabadilika dakika za mwisho, kitu ambacho tulikuwa tumekubaliana toka
Zanzibar, Rais mwenyewe naona kama kabadilika flani hivi, mimi nilikuwa
tayari kwenda kuifundisha Simba” >>> Morocco