Wananchi wa kijiji cha Saza wamefunga ofisi ya mwenyekiti wa kijiji hicho kwa kujenga matofali mlangoni.
huu ni mwonekano wa mlango wa kuingia katika ofisi ya mwenyekiti wa
kijiji cha Saza ambao wananchi wameamua kuufunga kwa kutumia matofali
ya kuchoma na saruji wakipinga Mwenyekiti huyo kuendelea kuwa
madarakani.
Akizungumza na ITV afisa mtendaji wa kata ya Saza Julius Simwita
amezitaja tuhuma ambazo zinatolewa na wananchi dhidi ya mwenyekiti wao
ambazo ndizo zimesababisha wachukue uamuzi wa kufunga ofisi hiyo.
Mgogoro huo ukamlazimu mkuu wa wilaya ya chunya Elias Tarimo kufika
katika kijiji cha Saza na baada ya kusikiliza madai ya wananchi hao
ikambidi amshauri mwenyekiti wa kijiji hicho kujiuzulu na kuitaka
halmashauri ya serikali ya kijiji kuteua mjumbe mmojawapo atakayekaimu
nafasi hiyo mpaka uchaguzi utakapoitishwa.