Serikali Kufanya Operasheni Nchi Nzima Ya Kukagua Vibali Vya Ajira Kwa Wageni
Serikali
imeamua muda wowote kuanzia mwezi huu kuanza ukaguzi wa vibali vya
Ajira za Wageni nchini, kufuatia muda wa siku 14 kuisha uliotolewa na
serikali katika tangazo la utolewaji wa vibali vya kazi kwa wageni
nchini lililotiwa saini Desemba 14 mwaka huu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Aiira, Vijana na Watu wenye ulemavu),
Jenista Mhagama (Mb), ambaye aliwataka waajiri wote nchini kwa muda wa
siku hizo wawe wametekeleza matakwa ya Sheria ya Kuratibu Ajira za
Wageni nchini Na. 1 ya Mwaka 2015.
“Katika
taarifa tuliyoitoa mwezi huu, tuliwajulisha waajiri wote wenye
waajiriwa wageni ambao wana vibali vya kazi za muda (Carry on Temporary
Assignment) na wale wote wasiokuwa na vibali vya ajira vilivyotolewa na
kamishna wa kazi nchini kuwa wanatenda kosa.
