Profesa Muhongo>> Nawahitaji Wala Rushwa Wote Wa Umeme
WAZIRI
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ameuagiza uongozi wa mkoa
wa Kagera,Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) na vyombo
vya dola, kuwashughulikia wala rushwa katika mradi ya umeme vijijini.
Amezitaka
taasisi hizo na uongozi huo, kuchunguza na kuwabaini wanaojihusisha na
vitendo hivyo katika mradi huo, unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini
(REA), ili wawachukulie hatua ikiwamo kuwafikisha mahakamani.