ONYO KALI LATOLEWA KWA WAKUU WA SHULE
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Mwanza, James William alisema kati ya wanafunzi 51,312
waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu, waliofaulu kuingia Kidato cha Kwanza ni
Jesse Mikofu, Mwananchi
Mwanza. Serikali mkoani hapa imewaonya wakuu wa shule zote kuwa yeyote atakayebainika
kuomba michango kwa wazazi itachukua hatua za kisheria.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkuu wa Mkoa huo, Magesa Mulongo.
Alisema Serikali imeanza kupeleka fedha za shule zote mkoani humo kulingana na mahitaji na
kwamba, atakayekwenda kinyume na agizo hilo la Serikali atakuwa amejifukuzisha kazi.
“Ukiona taasisi inakwenda kinyume na maagizo ya Serikali, jua msimamizi wake ni mzembe
hafanyi kazi yake, kwa wale watakaofanya hivyo tutawashughulikia kwelikweli,” alisema Mulongo.
Alisema watumishi wa namna hiyo siyo wa kuwavumilia, kwani ndiyo wanaowachonganisha
wananchi na Serikali, huku akiwataka wakurugenzi wa halmashauri na viongozi wengine wenye
mamlaka, kulisimamia suala hilo kwa umakini.