LOWASSA NAKOMAA MPAKA KIELEWEKE (KATUNI)

Katuni ilivyotafsiriwa na mhariri wa mtandao wa mjengwablog.com..
Msanii
amefanikiwa kufikisha ujumbe muhimu kuhusiana na maisha ya kisiasa.
Ieleweke, kuwa maisha ya kisiasa ni magumu. Hata hivyo, kama yalivyo
mengine, nayo huendelea.
Samwel Sitta katamka kuachana na siasa na atabaki kuandika vitabu. Huko nako kuna siasa. Mzee Sitta afuate nyayo ya Mzee Msekwa na hayati Baba wa Taifa, kwa kuwataja wachache. Hawa wamekuwa wakiandika makala za magazetini, si vitabu tu. Tatizo katika nchi yetu anayeandika makala gazetini husemwa kuwa ni mwandishi wa habari!

Kuna
waandishi wa habari na waandishi wa makala. Mzee Edward Lowassa yeye
hajakata tamaa, na mwanasiasa hupaswi kuwa mtu wa kukata tamaa. Hata
hivyo, kama Mzee Lowassa angeamua kuandika kitabu kuhusu maisha yake
kisiasa, basi, naamini kingesomwa sana.
Maggid,
Mwenyekiti/Mhariri
Mjengwablog.com(P.T)
Maggid,
Mwenyekiti/Mhariri
Mjengwablog.com(P.T)