EXCLUSIVE INTERVIEW: YAFAHAMU MAISHA YA KAMUSOKO NJE NA NDANI YA UWANJA, AMEKUWA NA MADEMU WANGAPI KABLA HAJAOA NA LINI ALIANZA KUPANDA NDEGE



Kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko
Kiungo wa Yanga Thaban Kamusoko
Jina la Thaban Kamusoko kwa sasa ni jina kubwa kwenye soka la Tanzania, huyu ni kiungo mchezeshaji wa timu ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam. Jamaa ni raia wa Zimbabwe ambaye kwa kifupi tunaweza kusema kwasasa ameanza kurejesha kitiTa cha mkwanja wa usajili Yanga walichotumia kumsajili kutokana na kazi yake anayoifanya uwanjani kuwa ni ya kutukuka.
Shaffihdauda.co.tz, imefanya exclusive interview na mchezaji huyo ili kujua ametokea wapi katika soka hadi amefika katika moja ya klabu kongwe hapa Tanzania (Dar Young Africans) na kufanikiwa kuonesha kiwango cha hali ya juu licha ya kuwepo kwa wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa kwenye kikosi hicho ambao ndiyo mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Shaffihdauda.co.tz: Unakumbuka lini ilikuwa ni mara yako ya kwanza kusaini mkataba kama mcheaji wa kulipwa?
Kamusoko: Mkataba wangu wa kwanza kabisa nilisaini na Njuen Sundowns na nilisaini mtaba wa miaka miwili na nusu japo nilitumikia kwa mwaka mmoja na nusu tu kwasababu kulikuwa na mvutano na timu yangu ya zamani.
Shaffihdauda.co.tz: Ulijisikiaje kupokea mshahara wako wa kwanza hasa unaotokana na kazi unayoipenda ?
Kamusoko: Nilijisikia vizuri sana, kwasababu kwa wakati huo ndiyo nilikuwa naomba siku zote na pia ukizingatia kuna wenzangu wengi ambao nilikuwa nao na walitaka kufikia nilipo lakini hawakufikia, kwahiyo mimi namshukuru sana Mungu.
Na mshahara wangu wa kwanza niliupeleka moja kwa moja kwa mama yangu mzazi na alifurahi sana kuona matunda ya kazi yangu kwasababu alijitolea sana ili mimi nifanikiwe.
Shaffihdauda.co.tz: Ni lini ilikuwa mara yako ya kwanza kupanda ndege, ulikuwa unaelekea wapi na hali ilikuwaje?
Kamusoko: Mara ya kwanza napanda ndege ilikuwa ni mwaka 2007 tukiwa tunakwenda South Africa kwenye mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (U20) COSAFA ilikuwa inafurahisha na kustaajabisha kiukweli mwili mzima ulikuwa unatetemeka na kuhisi mpira ndiyo utakuwa sehemu ya maisha yangu.
Shaffihdauda.co.tz: Lini ilikuwa mara ya kwanza kuwa na mpenzi na ku-kiss?
Kamusoko: Hayakuwa mabo yangu sana, lakini kama binadamu na mwanaume kuwa na mpenzi ni lazima na mpenzi wangu wa kwanza kabisa alikuwa anaitwa Posher anaishi South Africa kwa sasa. Sikumbuki sana lini hasa tulianza ku-kiss lakini nafikiri nilikuwa na umri wa miaka 17. Nakumbuka ilikuwa hatari sana wakati huo ukiwa na mpenzi kila mtu anashangaa umempataje.
Shaffihdauda.co.tz: Umewahi kuwa na wapenzi wangapi mpaka umekuja kukutana mkewako?
Kamusoko: Ni wengi sana, unajua ukiwa mwanaume wa shoka unaweza kuwa na mpenzi mmoja lakini ukaja kukutana na mwanamke mwingine mwenye sifa na vitu unavyovipenda unatamani uwenae.
Ukitaka ufaidi exclusive interview hii, unaweza kusikiliza audio kwa kubofya hapa chini na ku-enjoy kumsikiliza Thaban Kamusoko
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.