Watu Wanne Wapandisha Kizimbani Kwa Kusambaza Taarifa za Uongo Kwenye Mtandao wa Whatsapp
WATU wanne wakiwemo ndugu watatu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya kusambaza taarifa za uongo kwenye mtandao wa Whatsapp, kuwa nchi inaingia kwenye machafuko wakati wa uchaguzi.
Washtakiwa hao Leila Sinare (36), pamoja na ndugu watatu, Godfrey
Soka (45), Deo Soka (40) na Monica Soka (32), walifikishwa mahakamani
hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian
Mkeha.
Wakili wa Serikali Wankyo Simon akisaidiwa na Wakili Mwandamizi Mkuu
wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Johannes Kalungura, alidai kati ya
Oktoba 20 na 30 mwaka huu, kupitia mtandao wa Whatsapp, Leila alisambaza
ujumbe wa sauti uliokuwa na taarifa za uongo zenye lengo la kupotosha
jamii.
Alidai ujumbe huo ulikuwa unasema “ Ndugu zangu wa kigango cha siasa,
hakuna cha kutakiana uchaguzi mwema wala nini, nchi yetu inaingia
kwenye machafuko muda wowote kuanzia sasa hivi na kama tulivyoambiwa
nchi hii itageuka kuwa nchi ya vita, ni kweli imeingia kwenye vita.”
Taarifa hiyo inaeleza “maboksi yenye kura feki yamekamatwa, Jimbo la
Vunjo yamekamatwa matatu, tumekamata maboksi matatu yenye kura feki
Moshi mjini, maboksi sita Ilemela, Maboksi 12 Hanang, kwa kifupi
uchaguzi umeshavurugika na Tanga nasikia magari yamesimama sehemu,
makamanda wetu bado wanaendelea kufuatilia lakini inasemekana ni maboksi
ya kura na mpaka sasa hali siyo nzuri.”
Aidha, taarifa hiyo inaendelea kueleza “ CCM wameingiza kura nyingi
feki na niseme kutokana na hali halisi ambayo ipo hatuponi kwa sababu
Mwanza vijana wameshaanza kuuawa, wameshakufa vijana wanne, watano mpaka
sasa hali hiyo inaendelea…, CCM jamani tunaomba mtuachie nchi kwa
amani, kweli ingelipaswa kutuua angalau kwa sumu mkabaki wenyewe,
msitutese, msitutese…”
Wankyo alidai, Leila alisambaza ujumbe huo wa uongo kwa lengo la kuposha jamii kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Wankyo alidai, Leila alisambaza ujumbe huo wa uongo kwa lengo la kuposha jamii kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Katika mashitaka mengine yanayowakabili, ndugu watatu Godfrey, Deo na
Monica, alidai kati ya Oktoba 20 na 30 mwaka huu, Dar es Salaam, kwa
pamoja walisambaza ujumbe huo kupitia mtandao wa Whatsapp, group la
Soka, kwa lengo la kupotosha jamii kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Washtakiwa walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai upelelezi
wa kesi bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini hati ya Shilingi milioni tano. Kesi imeahirishwa hadi Desemba 3 mwaka huu.
Waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini hati ya Shilingi milioni tano. Kesi imeahirishwa hadi Desemba 3 mwaka huu.