Utambulisho wa msanii FEMI ONE (@Femi_One) kutoka KENYA na wimbo wa “WANJIKU KIMANI”

FEMI ONE
Msanii kutoka nchini Kenya chini ya uongozi wa Kaka Empire, anyeimba katika miondoko ya rap maarufu kama ‘Femione’ (pichani juu) anakuja na kibao chake kipya kinachojulikana kama ‘Wanjiku Kimani’ ambacho amekitambulisha hivi karibuni huko nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kibao hicho cha wanjiku kimani kinafanya vizuri sana pande za Nairobi na Kwenye mitandao kiujumla kwa kusikilizwa watu wengi sana.
HISTORIA FUPI YA MSANII FEMI ONE:
Femione alizaliwa Wanjiku Kimani huko nchini Kenya. Ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya kati ya watoto watatu. Yupo katika tasnia ya muziki kwa kipindi kirefu na hakuchagua rap bali rap ndio iliyomchagua.
SAFARI YAKE YA KIMUZIKI;
Femione alianza kurap akiwa na umri wa miaka 15. Alianza kufahamika alipojiunga na kundi lijulikanalo kama Young Star ikiwa na maana ya “Nyota Wadogo”, waliofundishwa namna ya kurap na kundi maarufu la marappa wa Kikenya liitwalo Wenyeji. Baada ya mafunzo hayo walihitimu na kufanikiwa kuunda kundi la watu watatu wote wakiwa wasichana. Kundi hilo liliundwa na Samantha, Mary and Femione kuanza kurap. Watatu hao walibahatika kutumbuiza katika matamasha kadhaa kama “WAPI” lakini watu walionyesha kuto tosheka nao baada ya show hiyo kuisha.
Wakati wa utumbuizaji wa tamasha la “WAPI” waandaaji wa tamasha hilo kutoka Afrika ya Kusini waliwaomba kuwa nao pamoja tena ili kwenda kutumbuiza katika tamasha kubwa huko Afrika Kusini lijulikanalo kama Fire on the Mountain kwa kipindi kile. Baada ya show hiyo ya Afrika Kusini Femione aliona kuwa anafursa nyingi kwa muziki anaoufanya.
Mara tu baada ya shoo nchini Afrika Kusini kundi la watatu hao lilivunjika kutokana kurudi tena masomoni. Mary alijotoa lakini Femione na Samantha walibaki pamoja mpaka ilipofikia wakati Samantha kuamua kufanya shughuli nyingine na kuachana na muziki.
Ijapokua Femione aliendelea kutumbuiza katika tamasha la WAPI ambapo King Kaka alipomuona, King Kaka alimuomba Femione kumshirikisha katika remix ya nyimbo yake ya “Ligi Soo” na baadae kufanikiwa kuwa remix nzuri kuliko zote nchini Kenya. Kipaji chake hapo ndio kikawa mwanzo wa kuzaa matunda na kufanikiwa kuingia mkataba na Lebo ya Kaka Empire na hata kuendelea kuwa maarufu zaidi.







Theme images by hanoded. Powered by Blogger.