TAZAMA HAPA ALIYOFANYA MAGUFULI PALE MUHIMBILI


Rais John Magufuli leo amefanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kujionea uhalisia wa huduma inayotolewa. 


Kama ilivyokuwa alipofanya ziara ya kushtukiza katika Wizara ya Fedha wiki iliyopita, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa hospitali hiyo na kuongozana nao katika maeneo ambayo aliyachagua yeye. 


Kabla ya kuelekea katika hospitali hiyo ya Taifa, Rais Magufuli alipita katika Hospitali ya Agha Khan kumjulia hali Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bi. Hellen Kijo Bisimba alinayepata matibabu katika hospitali hiyo baada ya kupata ajali ya gari jana katika makutano ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.