NUNUA MAFUTA KATIKA KAMPUNI YA GAPCO UNUFAIKE
Katika kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka huu, GAPCO, kampuni inayoongoza kwa uuzaji wa mafuta, imeamua kuwapa wateja wake zawadi ya kufungia mwaka. Katika kufanikisha hilo, kupitia mpango wake wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme ‘, kampuni imelenga kunufaisha na kuimarisha uhusiano wa kudumu na wateja wake kwa kuwapa mafuta ya bure.
Mpango huu unaoenda sambamba na promosheni ya ‘Jaza Mafuta na Ushinde’, umedhamiria kutoa lita 4,000 za petroli au dizeli za bure kwa wateja 100 watakao bahatika ndani ya wiki nne. Katika droo za kila wiki, kutakuwa na wateja 25 wanaoweza kujishindia lita 40 kila mmoja. Wateja wanaweza kujiongezea nafasi za ushindi kwa kujaza mafuta mara nyingi zaidi.
Pia, wateja ambao hawajajiunga na mpango wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme’ wanaweza kujiunga katika kituo chochote cha GAPCO kilichopo Dar es Salaam ili waweze kushiriki katika promosheni. Motisha zinazotolewa kupitia mpango huu, ni nje ya zawadi atakazoshida mteja katika promosheni, mteja wa GAPCO atajikusanyia pointi zitakazomwezesha kukomboa mafuta ya bure.
“Kupitia mpango huu wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme‘, tunataka wateja wetu wawe na furaha na waendelee kutumia bidhaa na huduma zetu. Mbali na kwamba tunatoa kadi hizi kwa mteja mmoja mmoja, pia tunaanzisha kadi kwa ajili ya makampuni na wasafirishaji. Kupitia kadi hizi, mbali na wateja kuweza kujikusanyia pointi zitakazomwezesha kupata mafuta ya bure, wateja wetu wataweza kudhibiti matumizi ya fedha zao,” alisema Meneja Masoko wa GAPCO, Caroline Kakwezi.
Mwanzoni mwa mwaka huu, GAPCO ilifanya mabadiliko makubwa na kuamua kujikita katika kujipambanua kwa namna ya kipekee. Katika mabadiliko haya, GAPCO iliboresha muonekano na mazingira katika vituo vyake vya mafuta vilivyopo Dar es Salaam. Ahadi ya kuwa na mafuta yenye ubora na ujazo wakuaminika, mazingira mazuri na rafiki, huduma bora inayojali mteja na ya haraka ni kati ya faida mahsusi anazopata mteja anayefika katika vituo
vya mafuta vya GAPCO nchini.
vya mafuta vya GAPCO nchini.
“Tukiwa na mtazamo na nia ya kuwapa wateja wetu maili nyingi zaidi na tabasamu zaidi, malengo yetu ya muda mrefu ni kuweza kupanua huduma zetu na kuhakikisha tunatoa huduma za ziada ili kuwaachia wateja wetu kumbukumbu sahihi ya huduma bora na za kisasa,” aliongeza Kakwezi.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (kushoto) akizungumza na wanahabari wakati wa kutangaza mpango wake wa ‘GAPCO Safari Loyalty ‘, unaolenga kuwanufaisha wateja wake kwa kuwapa mafuta ya bure, ulizindulia kwenye makao makuu ya Kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Jane Mwita.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi (kushoto) na Meneja wa Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Jane Mwita, wakionyesha vipeperushi vya Promosheni hiyo, mara baada ya kuizindua rasmi.