MVUA YALETA MAAFA HUKO ZANZIBAR
Paa
la jengo la Beit-al-ajab moja ya kivutio kikubwa cha utalii Zanzibar
limeanguka na kusababisha mtafaruku mkubwa kwa wakazi wa Mjimkongwe.
Paa hilo limeanguka baada ya kuwepo mvua na upepo mkali ambao
ulianza wakati wa asubui na paa hilo lilioko kwenye jengo hilo la
ghorofa tatu kuanguka chini na kuharibu gari tatu zilizokuwa zimeegeshwa
huku mshutuko huo ulisababisha watu kukimbia na kuacha mali zao za
biashara hata hivyo hakuna atahri za kuumia binadamu.
Wakiongea na Mtandao huu baadhi ya mashuuda walioshuudia paa hilo
likianguka wamesema ajali hiyo ilitokozea ghafla na kilichosaidia na
kwanza kuwepo kwa sauti ya mshtuko na baadaye ndio paa hilo likaanza
kuanguka hali hiyo ndiyo iliyosaidia watu waliokuwa wameketi chini na
wafanyabiashara za watalii.
Naye mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hifadhi wa Mjimkongwe Zanzibar
Bw Issa Sarboko akiongea na Mtandao wetu kwenye eneo la tukio amesisitiza kuwa
jengo hilo ni madhubuti na halijaathirika kilichotokozea ni kuwepo
mwanya wa upepo lakini mamlaka inalishugulikia ili kuondosha tatizo
lakini kwa hivi sasa jengo ilo limefungwa kwa ajli ya ukarabati.
Jengo hilo la Beita ajab ambalo ni moja ya kivutio kikubwa cha
watalii Zanzibar, hii ni mara ya pili ya kuwepo kwa ajali za kuporomoka
kwa jengo hilo ambalo limekuwepo zaidi ya miaka 100 na lilikuwa ni jengo
la ofisi kuu za serikali kabla ya mapinduzi na hivi sasa ni makumbusho
kubwa la historia ya Zanzibar.
source: Itv