Kama Unatafuta Kazi, Acha Kufanya Makosa Haya Ili Kuipata Kazi Hiyo.
Changamoto
ya ajira ni moja kati ya changamoto kubwa sana inayowakabili vijana
wengi hususani wanaomaliza masomo yao ya vyuo. Si ajabu sana kusikia
kijana yule kamaliza chuo kile lakini akiwa hana kazi. Hiyo ni
changamoto inayowakabili vijana wengi na ni kweli ipo na inasumbua.
Vijana wengi huzunguka huku na kule wakitafuta kazi bila kupata kazi
hasa hizo walizozisomea.
Pamoja
na changamoto hiyo kubwa ya ajira inayojitokeza, lakini kuna wakati
huwa yapo makosa yanayowafanywa na vijana wengi wanaotafuta kazi. Na kwa
makosa hayo hupelekea kukosa kazi hizo na kubaki mtaani kwa muda mrefu
sana bila ajira yoyote. Bila shaka umeshawahi kukutana au kuonana na mtu
ambaye yupo mtaani kwa muda merfu bila kazi yoyote.
Je,
umeshawahi kujiuliza tatizo kwa watu hawa hasa ni nini? Unaweza ukaja
na jibu rahisi tu na kuniambia hakuna kazi siku hizi. Hilo linaweza
likawa ni sawa, lakini je huo ndio ukweli halisi? Ukija kuchunguza kwa
makini utagundua watu hawa ambao wengi wao wanatafuta kazi kwa muda
mrefu bila mafanikio, wanafanya baadhi ya makosa ambayo yana wagharimu
kupata kazi hizo wanazozitafuta.
Je, unajua ni makosa gani ambayo watu hawa wanafanya na kuwanyima kazi hizo?
1. Kosa la kuchagua kazi sana.
Watu
wengi ambao wanajikuta wao ni wa kubaki mtaani kwa muda mrefu kosa
mojawapo kubwa wanalolifnya ni watu wa kuchagua kazi sana.
Mathalani,utakuta mtu amesomea digirii ya sociology (Mambo ya jamii),
lakini mtu huyu inapojitokeza kazi nyigine ambayo ingeweza kumuingizia
kipato tofauti na kile alichosomea inakuwa ni ngumu sana kwake kuifanya.
Kwa
mwendo huu wa kuchagua kazi siku hadi siku hujikuta ni watu wa kukosa
kazi kila kukicha. Hili najua unalijua vizuri na umeshakutana na watu wa
namna tena wengi tu, ambao wao ni watu wa kuchagua kazi nzuri, kazi
ambayo wanavigezo nayo kichwani mwao. Hilo si jambo baya ila angalia na
mzaingira ya wewe ulipo. Jitazame una kazi hadi kupelekea kuchagua kazi
sana, vinginevyo utaendelea kupigika mtaani bila kuwa na chohote.
Suluhisho
Najua
unailewa vyema hali ya maisha uliyonayo. Kama upo kwenye wakati wa
kutafuta kazi acha kutafuta sana kazi. Fanya kazi, kama ni uchaguzi
utaufanya ukisha pata kazi hiyo kwanza, itakayokufanya uishi.
![]() |
| UTAUMIA SANA KILA UNAPOIKOSA KAZI YA MSHAHARA MKUBWA |
2. Kosa la kutaka kazi ya mshahara mkubwa.
Wengi
wanaotafuta kazi na kujikuta kuzikosa ni watu wa kutafuta mshahara
mkubwa siku zote. Utakuta mtu hana kazi lakini inapotokea anapata kazi
hiyo shida inaanza kujitokeza kwenye mshahara. Anakuwa ni mtu wa
kupatanisha na kutaka mshara mkubwa ambapo waajiri wengi hupelekea
kushindwa kuwaajiri watu wa namna hiyo.
Kwa
mazingira kama hiyo inakuwa ni ngumu kupata kazi. Kwa namna yoyote ile
ili uweze kupata kazi ni muhimu kujifunza, kama hauna kazi tafuta kazi
kwanza. Acha kutafuta mshahara mkubwa. Kama utaendelea kutafuta mshahara
mkubwa, elewa utakosa kazi nyingi, na utaendelea kupishana na ajira
kila kukicha. Hicho ndicho kitu unachotakiwa kukiepuka kama upo kwenye
hali ngumu ya kutafuta kazi.
Suluhisho
Kwa
kipindi ambacho huna kazi acha kuangalia sana suala la mshahara.
Mshahara wako pengine utaongezeka zaidi hadi pale utakapotoa thamani
inayotakiwa.
3. Kosa la kutafuta eneo bora la kazi.
Pia
hili ni tatizo linawakabili vijana wengi kukosa kazi. Kuna watu
wanakuwa wanapata kazi lakini tatizo linakuja pale wanapoambiwa
wakafanye kazi katika eneo fulani, hapo ndipo inakuwa ngumu. Utakuta mtu
anaishi Dodoma lakini anapopata kazi nakuambiwa kazi hiyo ipo Tabora,
hapo ndipo ugumu unapoanza na kujikuta wanaachana na kazi hiyo.
Kwa
vijana walio wengi ukija kuangalia hayo ndiyo matatizo makubwa
yanayowapelekea kukosa kazi. Kama unafanya makosa hayo ni muhimu kwanza
kuyaepeka ili kujipatia kazi unayohitaji.
Angalizo
Ikiwa
utandelea kushikilia sababu hizo katika harakati zako za kutafuta kazi,
basi hakikisha una mbadala wa kukuingizia kipato, kinyume cha hapo acha
kusumbua watu kwa pesa za matumizi.
Karibu pia kwenye DIRA YA MAFANIKIO kuweza kujifunza na kujipatia maarifa ya kuboresha maisha yako.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani ngwangwalu,
Simu; 0713 048 035,
E-mail; dirayamafanikio@gmail.com
Blog; dirayamafanikio.blogspot.com
