Kwa mujibu wa chunguzi mbalimbali za masuala ya mahusiano zimebaini kuwa wasichana wengi zaidi huvutiwa sana na wanaume warefu kwa sababu zifuatazo 1.HALI YA KUJISIKIA SALAMA. Wasichana huhitaji mtu ambaye anajiamini na ambaye yuko tayari kumlinda kwa lolote lile litakalotokea,kwa miaka mingi imesadikika kuwa wanaume warefu wako katika nafasi nzuri zaidi ya kumlinda mpenzi wake. 2.WANA PENDA KUANGALIA MPENZI KWA JUU. Inasadikika kuwa wasichana hupenda wanaume warefu kwa sababu wanapenda kuangalia mpenzi kwa kuangalia juu,huwa wanajisikia faraja sana na ulinzi wa kutosha kutoka kwa mpenzi aliye mrefu kuliko mfupi. 3.WANAUME WAFUPI HAWAJIAMINI. Kwa sababu imejengeka kuwa wanaume warefu wanapendwa zaidi na wasichana,basi wao huwa hawajiamini wanapokutana na wapenzi wao na kujikuta wakifanya mambo ambayo wapenzi wao hawayapendi. 4.WANAUME WAFUPI WANA HASIRA. Huwa wepesi kukasirika kwa wapenzi wao wanapokosana hata kwa suala dogo tu. 5.HUWA WABISHI SANA NA HAWATOI NAFASI YA KUJIELEZA KWA WAPENZI WAO.