HUU NDIO UTABIRI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI,SOMA HAPA KUWAFAHAMU LIVE.
Dar
es Salaam. Baada ya kuapishwa kushika madaraka ya Rais, kibarua kizito
cha Dk John Magufuli ni kuunda Baraza la Mawaziri litakaloendana na kasi
ya kaulimbiu yake ya ‘Hapa kazi tu’, ambalo ni wazi litajaa sura nyingi
mpya.
Kujaa
kwa sura mpya katika baraza hilo kutokana idadi ya wabunge waliokuwa
mawaziri na naibu mawaziri katika Serikali iliyomaliza muda wake
kupungua kutoka 55 walioanza na Rais Jakaya Kikwete katika awamu yake ya
pili hadi 23, kati yao 20 wa majimbo na watatu wa viti maalumu
waliofanikiwa kurudi katika Bunge la 11.
Akizungumzia Baraza la Mawaziri linalotarajiwa, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema Rais Magufuli amekuwa waziri kwa miaka takribani 20, hivyo anajua kati ya mawaziri waliopita nani mzembe na nani mchapakazi, jambo ambalo litamfanya ateue watu sahihi.
“Tatizo
la nchi yetu ni mawaziri wanaoteuliwa, wengi wanajilimbikizia mali na
kuwa karibu na wafanyabiashara. Wapo wabunge walikuwa mawaziri wanaoweza
kwenda na kasi yake (Dk Magufuli).
“Kwanza
amejipa muda wa kutosha, hakutaka kuwahi kuteua, nadhani anajipanga ili
kupata watu sahihi. Watanzania watarajie mshangao katika uteuzi wake,
usisahau kuwa ana nafasi 10 za kuteua wabunge ambao anaweza kuwapa
uwaziri,” alisema.
“Anatakiwa kujitahidi kuwa na Baraza la Mawaziri ambalo halitakumbwa na kashfa kama ile ya Escrow au Dowans,” alisisitiza.
Kwa
upande wake Profesa wa Uchumi katika Kilimo wa Chuo Kikuu cha Sokoine
(SUA), Damian Gabagambi alisema tatizo la Tanzania si sera wala sheria
mbovu, akifafanua kuwa hata Dk Magufuli alipokuwa Waziri wa Ujenzi
aliweza kufanya mambo mazuri.
“Naona
tatizo ni uzembe tu na umakini. Dk Magufuli aliwahi kusema kuwa
ataingia mikataba na mawaziri wake ili kama wakishindwa kutekeleza jambo
awawajibishe. Nadhani hili ni wazo zuri.
“Yule
atakayeshindwa akae pembeni. Pia anatakiwa kuteua watu wasio na kashfa,
nadhani uzoefu wake serikalini umempa mwanga na sasa atakuwa anawajua
mawaziri wazembe na wachapakazi,” alisema.
Alifafanua kuwa baraza hilo linapaswa kuchanganywa mawaziri wapya na wa zamani wachache, ili kuondoa “kufanya kazi kwa mazoea”.
Hadi
anaondoka madarakani, Rais Jakaya Kikwete katika baraza lake alikuwa na
mawaziri na naibu mawaziri 55, wakiwamo 16 ambao alianza nao tangu
2005.
Kati
yao, mawaziri 12 walishindwa kura ya maoni ndani ya CCM, sita
waliangushwa katika Uchaguzi Mkuu, watatu walikuwa wabunge wa kuteuliwa
na rais na hawakugombea, wawili walifariki dunia na sita hawakugombea
ubunge.
Katika
orodha hiyo, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Saada Mkuya baada ya kuteuliwa
na Rais Kikwete kuwa mbunge, amegombea ubunge katika Jimbo la
Kijitoupele, Zanzibar ambalo bado halijafanya uchaguzi.
Pia
mawaziri waliobahatika kurudi bungeni ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na Watoto, Sofia Simba, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki na Naibu waziri wa Katiba na sheria,
Ummy Mwalimu.
Katika orodha ya mawaziri 55 yupo Dk Magufuli na Samia Suluhu Hassan waliochaguliwa kuwa Rais na Makamu wa Rais.
Katika
uteuzi wake, Rais Magufuli anaweza kurejesha baadhi ya wabunge
waliokuwa mawaziri, pia kuchagua wabunge nje ya hao au kuteua ambao sasa
siyo wabunge, lakini vyovyoite hawatarajiwi kuwa wengi.
Pia,
Dk Magufuli anaweza kutumia utaratibu uliomwibua yeye, wakati wa Rais
mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alipoteua sura nyingi mpya za
wabunge na kuwapa uwaziri.
Pia
upo uwezekano wa kuteua wabunge wapya kimikoa au kikanda uliokuwa
unatumiwa na mtangulizi wake ambao utakumbwa na changamoto kutokana na
baadhi ya mikoa kuwa upungufu wa wabunge wa chama chake.
Mkoa
wa Kilimanjaro mathalan, waliokuwa mawaziri watatu wameshindwa ubunge,
akiwamo Anne Kilango (Naibu-Elimu), Aggrey Mwanri (Naibu-Tamisemi) na
aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda, Dk Cyril Chami, huku wakibaki mawaziri
wa zamani mawili.
Endapo
Dk Magufuli atafuata utaratibu wa kimikoa, nyota inaweza kuwawakia tena
Profesa Jumanne Maghembe (Mwanga) na aliyekuwa waziri wa Uvuvi na
Mifugo, Dk David Mathayo David aliyevuliwa uwaziri katika sakata la
Operesheni Tokomeza.
Wadadisi
wa masuala ya kisiasa wanajiuliza endapo pia, Rais Magufuli anaweza
kuwakumbuka mawaziri waliotoswa kutokana na kashfa ya Akaunti ya Tegeta
Escrow, Profesa Anna Tibaijuka (Ardhi) na Profesa Sospeter Muhongo
(Nishati na Madini).
Charles
Mwijage (Naibu-Nishati na Madini), Stephen Masele (Naibu-Muungano),
William Lukuvi (Ardhi), Mwigulu Nchemba (Naibu-Fedha), Jenista Mhagama
(Sera, Uratibu Bunge), Gerson Lwenge (Naibu-Maji).
Waliokuwa mawaziri ambao waliangushwa kura ya maoni Dk Binilith Mahenge (Mazingira), Adam Malima (Naibu-Fedha), Dk Seif Rashid (Afya), Dk Pindi Chana (Naibu-Wanawake, Jinsia na Watoto), Dk Titus Kamani (Uvuvi), Kaika Telele Naibu-Uvuvi) na Amos Makala (Naibu-Maji).
Dk
Abdulla Juma Abdulla (Naibu-Afrika Mashariki), Mathias Chikawe (Mambo
ya Ndani), Mahadhi Juma Maalim (Naibu-Mambo ya Nje), Pereira Ame Silima
(Naibu-Mambo ya Ndani), Christopher Chiza (Uwekezaji na Uwezeshaji) na
Gaudencia Kabaka (Kazi na Ajira).
Mawaziri
waliokuwa wabunge wa viti maalumu ambao wamerudi mjengoni, Sofia Simba
(Wanawake, Jinsia na watoto), Angela Kairuki (Naibu-Ardhi) na Ummy
Mwalimu (Naibu-Katiba na Sheria).
Mawaziri
walioangushwa katika uchaguzi ni Dk Stephen Kebwe (Naibu-Afya), Anne
Kilango- Malecela (Naibu-Elimu), Dk Fenella Mukangara (Habari), Aggrey
Mwanry (Naibu-Tamisemi), Stephen Wasira (Kilimo), Godfrey Zambi
(Naibu-Kilimo).
Mawaziri
ambao hawakugombea kabisa ubunge ni Samuel Sitta (Uchukuzi), Profesa
Mark Mwandosya (Ofisi ya Rais-Kazi Maalumu) Bernard Membe (Mambo ya
Nje), aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Dk Makongoro Mahanga
aliyehama CCM na kujiunga na Chadema.