Nashukuru
kwa heshima aliyonipa mtumishi wa Mungu, T.B Joshua kwa kuja nyumbani
kujadili mambo ya taifa, na baadaye kushiriki kwenye sala na ndugu na
familia. Mungu atuongoze. Mungu ibariki Tanzania!"-Edward Ngoyai
LowassaMaelezo kwa mujibu wa tovuti ya John Kitime
(johnkitime.co.tz)Temitope Balogun Joshua (T.B. Joshua) alizaliwa tarehe
12 Juni 1963, katika kijiji kidogo cha Arigidi kilichoko Akoko, Jimbo
la Ondo, Nigeria. Inasemekana mama yake alikaa na mimba kwa miezi 15,
kabla Temitope hajazaliwa.Katika kabila lake kulikuweko na hadithi ya
zaidi ya miaka 100 ambayo ilitabiri kuwa kuna mtoto atazaliwa katika
familia masikini, ambaye Mungu atamtumia sana, na wengi kule kwao
huamini kuwa Temitope ndie aliyetajwa katika utabiri huo. Siku tatu
baada ya kuzaliwa kwake, jiwe kubwa lilirushwa kutoka kwenye sehemu
kulikokuwa kunapasuliwa mawe, jiwe hilo lilitoboa bati na kumkosa kosa
Temitope kwa sentimita chache. Na ndipo mama yake alimpa jina la
Temitope, likiwa na maana ‘Ulichonipa Mungu lazima kishukuriwe’.Jina
analojulikana sana sasa ni T. B. Joshua.TB Joshua ni muhubiri
mwanzilishi na kiongozi wa The Synagogue, Church of All Nations (SCOAN),
hii ni taasisi ya kidini inayoendesha Emmanuel TV, Tv ambayo huonekana
kote duniani ikiwa inarushwa kutoka Lagos Nigeria. TB Joshua anasemeka
ni moja ya watu 50 wenye ushawishi zaidi Afrika, anajulikana sana kwenye
mitandao ya Facebook ambako anawafuasi zaidi ya milioni moja laki tano,
na video zake nyingi zilizomo kwenye Youtube. Kwa mujibu wa Forbes,
mwaka 2011 TB Joshua alikuwa mtu wa tatu kwa utajiri nchini
Nigeria.Wakati akiwa shule alijulikana kwa jina la Balogun Francis,
alisoma shule ya St. Stephen’s Anglican Primary School ya Arigidi-Akoko,
kati ya mwaka 1971 na 1977, lakini hakumaliza sekondari. Wakati yuko
shule alijulikana kama “small pastor” kutokana na kupenda sana biblia,
baada ya kuacha shule alifanya kazi mbalimbali ndogo ndogo, hatimae
akaanzisha darasa la biblia kwa watoto, wakati huohuo akaanza
kujiendeleza kwa masomo ya jioni. Hatimae akaamua kwenda kujiunga na
jeshi la Nigeria, lakini kwa bahati mbaya akaachelewa treni kwenda
kwenye usaili na hivyo ndoto hiyo ikaishia hapo.Kwa maelezo yake
mwenyewe anaeleza jinsi alivyokabithiwa upako wake, “ Nilikuwa katika
hali ya kuzimia kwa siku tatu mfululizo, nikaona mkono ukielekeza Biblia
kwenye moyo wangu, na Biblia ikaingia kwenye moyo wangu na moyo wangu
wa zamani ukachanganyika na Biblia. Ufahamu uliponijia nikawaona Mitume
na Manabii wa zamani wako na mtu ambaye sikuweza kuona kichwa chake kwa
sababu alikuwa mrefu sana amefika mpaka mbinguni. Nikaamini kuwa alikuwa
ndie Bwana wetu Yesu Kristo, nami nikajiona nimo katika hawa Manabii na
Mitume wa zamani.Nikauona mkono wa yule mtu mrefu sikuweza kuona uso
wake maana ulikuwa na mwanga mkali sana sikuweza kabisa kuangalia uso
wake. Lakini Mitume wengine niliweza kuwaona. Mitume Peter na Paul,
Manabii Moses, Eliya na wengine, kwani majina yao yalikuwa yameandikwa
kwa herufi kubwa vifuani mwao. Nikasikia sauti inasema, “Mimi ni Mungu
wako, nakupa upako nenda kafanye kazi ya baba yako wa mbinguni.”Wakati
huohuo yule mtu mrefu akanipa Msalaba na Biblia iliyokuwa kubwa kuliko
ile iliyoingia moyoni mwangu. Akaniahidi kuwa kila nitakapo tumia muda
wake na jina lake nitapata Msalaba mkubwa zaidi, nikienda kinyume na
mambo yatakuwa kinyume. Nikasikia sauti ya yule mtu mrefu ambaye sikuwa
naweza kuona kichwa chake ikasema,’ Mimi ndie Bwana wako, niliyekuwa na
ambaye ndie, mimi ni Yesu Kristo ninaetoa amri kwa mitume na manabii
wote. Sauti ile ikasema tena ‘Nitakuonyesha mambo mazuri ya ajabu na
nitajionyesha kupitia mafunzo, mahubiri, miujiza, ishara, kwa ajili ya
kuokoa roho za watu. Kutoka wakati huo nimekuwa napata maono kila mwaka
na Msalaba mkubwa zaidi ukiwa na maana majukumu makubwa zaidi”SCOAN ina
tawi moja tu nalo liko Ghana, kwa sasa kila Jumapili kuna ibada Nigeria
ambayo huhudhuriwa na kiasi cha watu 15,000 kila Jumapili. Uponyaji ni
kati ya mambo mengi yanayofanywa katika kanisa la TB Joshua watu wengi
wamekuwa wakisema wamepona maradhi mbalimbali kutokana na kufika
kanisani hapo na kwa kutumia maji, ‘annointed water’ ambayo hutolewa na
TB Joshua.Wakati wa tatizo la Ebola TB Joshua alisema maji hayo yanaweza
kutibu ugonjwa huo na alituma chupa 4,000 za maji hayo zikiambatana na
dola 50,000 kwenye serikali ya Sierra Leon. Hili lilikuja hasa baada ya
maafisa afya wa Lagos walipomtembelea TB Joshua kumtaka asiwaruhusu
wagonjwa Ebola kuja katika kanisa hilo kwa kuondoa uwezekanao wa kupata
mlipuko wa ugonjwa huo katika jiji hilo. Wasanii wa Nollywood kama Jimmy
Iyke na Camilla Mberekpe pia ni kati ya watu wengi waliowahi kupata
huduma za kuondoa mapepo katika miili yao katika kanisa hilo.Pia TB
Joshua anasemekana ameweza kutabiri mambo mengi ikiwemo kifo cha Michael
Jackson, milipuko ya Boston na hata matokeo ya mechi mbili za fainali
za AFCON, ambapo moja mshindi alikuwa Zambia na nyingine Nigeria
ilichukua ushindi. Amesha wahi kutabiri kuhusu kifo cha Rais mmoja wa
Afrika na inasemekana Bingu Mutharika wa Malawi ndie aliyetabiriwa
wakati huo. Pia anasemekana kutabiri kuhusu ndege ya Malaysian Airline
iliyopotea baharini, miezi kadhaa kabla ya tukio hilo. [1.6MB]VIDEO CHAFU YA WANACHUO WA UDSM YAVUJA IONE HAPO CHINI