CHADEMA KUPINGA MATOKEO MAHAKANI
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Katibu wa
Chadema wilayani humo, Fabian Moke, alisema kutokana na hali hiyo chama
hicho kinajiandaa.
kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo. Alisema kufuatia kasoro
hizo, wagombea wote wa chama hicho katika maeneo hayo waligoma kusaini
matokeo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi. “Tumeitisha
kikao cha dharura cha viongozi ngazi ya wilaya na jimbo ili kueleza
hali hiyo ya sintofahamu kwa wanachama wetu,” alisema Moke.
Hata hivyo, msimamizi wa uchaguzi wilayani humo, Mohamed Maje,
alisema sheria ya uchaguzi haikatazi kutangaza matokeo hata kama mgombea
kagoma kusaini, bali anachotakiwa kufanya mgombea huyo ni kufuata
taratibu za kisheria kutafuta haki yake.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, George
Lubeleje (CCM) aliibuka mshindi wa nafasi ya ubunge Jimbo la Mpwapwa kwa
kupata kura 32,208 sawa na asilimia 74.46, huku nafasi ya udiwani CCM
ikishinda kata zote 15.
Kwa upande wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene (CCM) ambaye
pia ni Waziri wa Nishati na Madini, alitangazwa mshindi wa nafasi hiyo
kwa kupata kura 37,327 sawa na asilimia 81, huku kwenye udiwani CCM
kikishinda viti vyote 18.
CHANZO:
NIPASHE