Bado Nitaendelea Kufanya Muziki - Professor Jay

Mbunge mteule wa Mikumi kipitia tiketi ya CHADEMA, Joseph Haule aka Professor Jay, amesema ataendelea kufanya muziki hata akiwa bungeni kwa sababu ndio kitu kilichomfikisha hapo alipo.

Professor amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa ataendelea kukiheshimu kipaji chake licha ya kupata tiketi ya kuingia bungeni.
“Muziki niliokuwa nikiufanya na ninaoendelea kuufanya ni sauti ambayo nilikuwa nikiipaza kwa ajili ya ustawi wa taifa langu na mustakabali wa nchi yangu. Nimeimba vitu vingi kuhusiana na changamoto zinazotukabili katika maisha yetu, so muziki umefanya niweze kupata sauti na kusikika zaidi,” amesema.
“Kwahiyo muziki umeplay role kubwa ya mafanikio haya maana nisingejulikana bila muziki, nitaendelea kuheshimu muziki na ni kipaji ambacho nimepewa na Mungu hata kama naingia mjengoni nitaendelea kufanya muziki,” ameongeza.

Aliyekuwa mpenzi  wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi, Faiza Ally ameamua kuweka wazi kuwa japokuwa wamegombana na mzazi mwenzake  lakini bado anampenda na kumthamini.
Kupitia kwenye akaunti yake wa instagram amepost picha ya Sugu na kuandika
“Alie kwambia simpendi nani ???? Nampenda ndio maana nili zaa nae  na sio lazima nilale nae na kuamka nae ndio mjue nampenda – unaweza unampenda mtu kwa mbali na bado ukasimama kwenye ukweli tu – kwa mimi that’s true love – oh yes nampenda na nina mpenzi tunapenda ! So what?????” aliandika.


MillardAyo.com
Jamjicho Newzz
Theme images by hanoded. Powered by Blogger.