Tajiri wa Afrika ataka kuinunua Arsenal
Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote anaamini ujenzi wa kampuni ya mafuta nchini kwake utampa fedha za kutosha kuinunua klabu hiyo.
Dangote, 58, anayekadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 11.5, anasema amekuwa mshabiki wa The Gunners tangu miaka ya 1980.
“Tutakapokamilisha kampuni hii, nitakuwa na muda wa kutosha na vyanzo vya kutosha kulipa wanachokitaka,” aliiambia BBC Hausa.
Mmarekani Stan Kroenke ndiye mwenye hisa nyingi, anamiliki hisa asilimia 66.64 za kampuni mama ya Arsenal Holdings pls. Mrusi Alisher Usmanov anamiliki hisa asilimia 29.11.
Dangote anashika nafasi ya 67 katika orodha ya matajiri Forbes.